Saturday, June 18, 2016

Rama D na Lady Jay Dee vipiiiii???


Mwanamuziki wa R&B nchini Tanzania Rama D, amekanusha vikali habari zilizotapakaa mtandaoni kwamba kwa sasa anatoka kimapenzi na mwanadada Lady Jay Dee, amesema wanaheshimiana sana na haiwezi kutokea kitu kama hicho daima .

Hata hivyo Rama D ameendelea kusema kwamba yeye anamfahamu mpaka mpenzi wa mwanadada Lady Jay Dee na kusema hata siku ya show ya 'Naamka Tena Concert' alipanda jukwaani kuonesha jinsi anavyomkubali mwana dada huyo.

Rama D anasema anawashangaa sana watu wanaoenda kufanya video zao nje na kusema kwamba haoni sababu ya kufanya video hizo nje kwani hapa nyumbani kuna mazingira ya kutosha kufanya video nzuri zitakazoitangaza nchi.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!