Wednesday, June 22, 2016

Serikali yaahidi kupambana na ugonjwa wa homa ya manjano nchini


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania imesema kuwa imejipanga kupambana na ugonjwa wa homa ya manjano kwa kuandaa timu za wataalam, vifaa tiba na chanjo za kutosha kuweza kukabiliana na ugonjwa huo endapo utajitokeza nchini.


Msemaji wa Wizara Nsachris Mwamwaja amesema pamoja na jitihada za serikali ni vyema wananchi wenyewe wakajitokeza mapema hospitali pindi wanapobaini kuwa na dalili za ugonjwa wa homa ya ini.

Mlipuko wa homa ya manjano umesababisho vifo vya watu 138 nchini Angola, na nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako ugonjwa huo umeripotiwa kuuwa watu kadhaa, na nchini Kenya mtu mmoja amefariki dunia.

Mwamwaja ametaja dalili za ugonjwa huo kuwa ni pamoja na kutokwa na damu sehemu za wazi kama mdomoni, pua, macho na tumboni na wakati mwingine damu huonekana kwenye matapishi na kinyesi na baadaye figo kushindwa kufanya kazi.

Dalili nyingine ni maumivu ya misuli pamoja na mgongo, mwili kutetemeka, kupoteza hamu ya kula, kusikia kichefuchefu na kutapika, mwili kuwa na manjano ambapo amewataka wananchi kuzingatia usafi ili kuondoa uwezekano wa mazalia ya mbu waenezao ugonjwa huo.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!