Wednesday, June 15, 2016

Serikali yapiga marufuku uuzaji wa damu salama


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema Taifa lina uhaba mkubwa wa damu salama lakini wananchi hawana mwamko wa kuchangia damu kwa kuwa hata kama wakichangia wanapokuwa na wagonjwa hutakiwa kunua nudamu hiyo.

Akizungumza leo kwenye maadhimisho ya kuchangia damu salama yaliyofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Nyerere Square Mwalimu alisema kuwa tabia ya waganga Wakuu wa Hospitali za Wilaya na Mikoa kuwauzia damu wagonjwa ndio chanzo kikubwa kunachopelekea wananchi kutokuwa na moyo wa kuchangia damu.

Ametoa wito kwa waganga wote waliopo kwenye vituo vya afya vya serikali na hospitali zote za mikoa nchini kuweka mabango yanayoelezea kuwa damu haiuzwi bali inatolewa bure.

Kwa upande wake meneja wa mpango wa damu salama nchini, Dk, Abdul Juma amesema kuwa taifa bado lina changamoto kubwa ya uhaba wa damu salama hali inayohatarisha uhai wa watoto wadogo, akina mama wajawazito na majeruhi wa ajali mbalimbali.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!