Monday, June 20, 2016

Shamsa Ford-Vimini vyangu Havihusiani na Malezi ya Mtoto wangu..


DIVA mwenye ‘title’ kubwa Bongo, Shamsa Ford amesema kuwa tangu awe mzazi anajitahidi kuishi maisha ya kistaarabu sana kiasi kwamba hahitaji kuwa na skendo ili kuitunza heshima yake kwa mwanaye wa kiume aitwaye Terry pale ambapo atakuwa kijana.


Shamsa alisema hayo wakati akipiga stori mbili-tatu na mwandishi, aliulizwa kwa nini anapendelea kuvaa mavazi mafupi alisema kuwa hiyo ni ‘hobby’ yake tangu utotoni, kila mmoja kwenye familia yake anafahamu hilo na wala haihusiani kabisa na malezi ya mtoto.

“Mimi nililelewa na mama yangu mkubwa ambaye ameolewa na Mzungu, tangu udogoni alikuwa ananivalisha nguo fupi pamoja na watoto wake. Kwenye familia yetu suala hilo si tatizo wala halihusiani na malezi ya mtoto, ninaimani hata Terry akikua ataliona kuwa ni jambo la kawaida kabisa,” alisema Shamsa.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!