Sunday, June 12, 2016

TRA wameendeleza jitihada za kuanzisha jumuiya za wanafunzi wa kodi vyuoni


Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) katika kuhakikisha elimu na uhiari wa wananchi kupenda kulipa kodi unaongezeka nchini wameendeleza jitihada zake za kuanzisha jumuiya za wanafunzi wa kodi vyuoni ili kuandaa vijana waweze kutimiza wajibu wao pindi watakapoanza kupata mapato.

Akizungumza katika ufunguzi wa jumuiya ya wanafunzi wa kodi vyuoni katika chuo cha kodi, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, RICHARD KAYOMBO, amesema hatua hiyo ni baada ya kuanzisha mfumo wa vilabu vya kodi kwenye shule za sekondari kuonesha mafanikio hivyo mamlaka ya mapato ikaona umuhimu wa elimu hiyo kufika katika ngazi za vyuo ili kutoa fursa kwa wanavyuo kuweza kujadili mambo mbalimbali ya kodi wakiwa katika mazingira yao ya vyuo.

Jumuiya hizo zinapaswa kuhakikisha zinaongeza uelewa na uhiari wa wananchi kupenda kulipa kodi pamoja, taratibu na sheria za kodi kueleweka vyema kwa jamii pamoja na kuongeza wigo wa kodi kwa kuibua vyanzo vipya vya kodi, huku Mamlaka ya Mapato Tanzania ikiwa na majukumu ya kutoa elimu ya kodi kwa wanachama ili waweze kuelewa sheria za kodi zinazosimamiwa na mamlaka ya mapato Tanzania pamoja.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!