Wednesday, June 22, 2016

Ukosefu wa Lift katika hospitali ya Muhimbili imekua Kero kubwa kwa Wagonjwa na Wauguzi

Ukosefu wa Lift katika jengo la wagonjwa la taasisi ya mifupa ya MOI katika Hospitali kuu ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam umeelezwa kuwa moja ya changamoto kubwa inayowakabili wagonjwa wanaofika katika kitengo hicho kwa ajili ya kupata matibabu.

Muonekano wa jengo bora na imara la kitengo cha mifupa katika hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam, ambalo ukosefu wa lift licha ya kuwa mwiba kwa wagonjwa.
 
Ambapo  mmoja wa wauguzi wa jengo hilo ambaye tunahifadhi jina lake ameeleza kuwa madhara wanayoyapata kuwapandisha wagonjwa kutoka ghorofa ya kwanza hadi ya tano kwa kutumia ngazi.
 
Huku tukipiga picha kwa usiri, tulizungumza na mmoja wa mafundi wa kampuni ya Premider Elevetor ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake ambapo amesema wameamua kusitisha utoaji huduma wa Lift kutokana deni kubwa wanaloidai taasisi hiyo, na kwamba watafanya hivyo mpaka pale deni lao litakapolipwa.
 
Lakini uongozi wa taasisi hiyo ya mifupa ya MOI umesisitiza hakuna tatizo la Lift katika jengo hilo,huku wagonjwa wakisema Lift ni changamoto kuu kwa wiki sita sasa.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!