Friday, June 17, 2016

Watu wanne wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za ujambazi mkoani Kilimanjaro.


Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu wanne wanaosadikiwa ni majambazi wa kutumia silaha za moto,na jadi kuvunja maduka katika maeneo mbalimbali ya mkoa kilimanjaro.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Bw.Wilbroad Mtafungwa amesema matukio ya ujambazi wa kutumia silaha,kuvamia maduka na kupora bidhaa mbalaimbali fedha na kurejuhi watu yameongezeka katika mkoa wa Kilimanjaro.
 
Amesema watuhumiwa hao wamekatwa na silaha bunduki aina ya Shortgun ,bidhaa mbalimbali,silaha za jadi wanazotumia kuvunja maduka hali ambayo imesababisha wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro kuishi kwa wasiwasi.
 
Kamanda Mtafungwa anasema baada ya kukamatwa kwa majambazi hao wameeleza jinsi wanavyotumia silaha hizo kufanya uhalifu na kuwataka wananchi kuendelea kuwafichua wahalifu katika maeneo wanayoishi ili hatua zaidi zichukuliwe.
 
Na mmiliki aliyeporwa Bunduki hiyo inayotumika kwenye matukio ya ujambazi Bw.Basil Mosha mkazi wa kijiji cha Rosho Kilema Marangu anasema siku ya tukio watu hao walimvamia nyumbani kwake majira ya usiku na kuwajeruhi yeye na mke wake na kisha kuondoka na silaha hiyo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!