Monday, June 20, 2016

Watumishi wanne Mtwara kufikishwa mahakamani


Mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego, ameamuru kukamatwa na kufikishwa mahakamani watumishi wanne wa Idara ya Manunuzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba, kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha wakati wa mchakato wa zabuni ya kutafuta mkandarasi wa ujenzi wa barabara za halmashauri na kuisababisha halmashauri hiyo hasara ya kiasi kubwa cha fedha.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2014/2015, Bi. Dendego amesema vitendo vilivyofanywa na watumishi hao ni kinyume cha sheria hivyo amemwagiza mkuu wa wilaya kuhakikisha wanakamatwa.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Namkulya Salum amewataja watuhumiwa hao kuwa Afisa Manunuzi wa Halmashauri Michael Ngajua na Afisa Mifugo Robert Mwanawima, ambao maadhimio ya kukamatwa kwao yametokana na mapendekezo yaliyotakana na hoja iliyowasilishwa mbele ya wajumbe na Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo Bw. Ally Machela.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!