Tuesday, June 28, 2016

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza kuteuliwa Septemba 2


Waziri Mkuu mpya wa Uingereza, atateuliwa Septemba 2.Tarehe hiyo imetangazwa Jumatatu hii na kamati maalum inayosimamia upatikanaji wa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo baada ya David Cameron kutangaza kujiuzulu wiki iliyopita.

“We recommend that the process of electing a new leader of the Conservative Party should commence next week … and conclude no later than Friday the second of September,” alisema Graham Brady, mwenyekiti wa kamati hiyo.

Cameron alitangaza kustaafu baada ya Uingereza kuamua kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, EU.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!