Wednesday, June 29, 2016

Wizara ya Elimu yazindua mpango wa kuboresha shule kongwe nchini.


Serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi imefuta maadhimisho ya wiki ya elimu nchini badala yake imezindua mpango wa kuimarisha shule zote kongwe zilizoweza kuzalisha wataalamu mbalimbali ili kuendelea kukuza elimu na kurudisha sifa na uwezo wa shule hizo.

Mpango huo unaolenga kukuza elimu nchini umezinduliwa mkoani Morogoro na waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Prof.Joyce Ndalichako wakati wa utoaji wa zawadi kwa wanafunzi, shule, halmashauri na mikoa iliyofanya vizuri kwenye masomo na kupata ufaulu  wa hali ya juu  ikiwa ni sehemu ya kutoa motisha ambapo ametoa zawadi za fedha taslimu vyeti na tuzo kwa shule hizo ambapo katika mikoa na halmashauri zilizofanya vizuri kitaifa zimeongozwa na mkoa wa Katavi  huku akibainisha wiki ya elimu ambayo imefutwa rasmi ilikuwa ikisababisha upotevu wa fedha nyingi kutokana na takribani bilioni 1.2 kutumika katika maadhimisho hayo badala yake sasa fedha hizo zitaelekezwa kuboresha miundombinu katika shule zote nchini kwa kuanza na shule zote kongwe.
Mkurugenzi wa usimamizi wa elimu kutoka TAMISEMI Mwl.Juma Japhet amesema wako tayari kushirikiana kikamilifu na wizara hiyo katika kuboresha miundombinu ya shule na kutatua changamoto za walimu nchini huku mkuu wa shule ya sekondari ya Mzumbe ambayo ni miongoni mwa zilizopata tuzo, alikiri kuwepo kwa changamoto ya miundombinu na vifaa ingawa akataja mbinu wanazotumia kufanikisha kutoa elimu bora.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!