Sunday, June 12, 2016

Wizara za Mawasilino, Elimu na TAMISEMI Zakanusha Taarifa Zilizozushwa kuwa Ajira za Waalimu Zimesitishwa

 Makatibu wakuu wa wizara za Mawasilino, Elimu na TAMISEMI nchini Tanzania wamezitaka mamlaka husika ikiwemo ya jeshi la polisi kumbaini mtu aliyesambaza taarifa walizodai ni za upotoshaji zinazosema kuwa ajira za ualimu kwa mwaka 2015-2016 zimesitishwa.

Wakizungumza kwa pamoja leo jijini Dar es salaam makatibu hao wamesema taarifa hizo zilizopo kwenye mitandao ya kijamii zina lenga kuleta chuki baina walimu hao na serikali, jambo ambalo ni lazima wahusika watafutwe na kuchukuliwa hatua.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Faustini Kamuzora amesema wizara yake imeanza kulifanyia kazi suala hilo na itahakikisha aliyehusika kusambaza taarifa hizo za uongo anabainika na kuchukuliwa hatua.

Amesema sheria ya makosa ya mitandao ndiyo itatumika katika kumtafuta na kumkamata huku akisisitiza kwa watumiaji wa mitandao kuitumia teknolojia hiyo kwa malengo mazuri na sio vinginevyo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!