Monday, June 27, 2016

Zoezi la uhakiki wa vyama vya Siasa kuanza leo kwa vyama vilivyopo Dar


Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Uhakiki wa Vyama vya Siasa  Bwana. Sisty Nyahoza ameanza zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini  Dar es Salaam leo.

 
Bw.Willy Brown Nyantiga, Mhasibu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini akihoji taarifa za fedha wakati wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa kwa chama cha NLD Jijini Dar es Salaam leo . Katikati ni Mwenyekiti wa chama , Bw. Oscar Emmanuel Makaidi na Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Tozzy Ephraim Matwanga ( kulia)


Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Uhakiki wa vyama vya Siasa , Bw. Sisty Nyahoza (kulia) akihakiki daftari lenye orodha ya wanachama wa Chama cha National League for Democratic (NLD) wakati wa zoezi la kuhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho Oscar Emmanuel Makaidi na Katibu Mkuu wa NLD Tozzy Ephraim Matwanga.


Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Ibrahim Mkwawa (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU) wakati wa zoezi la kuhakiki utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam leo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!