Wednesday, July 27, 2016

Aunt Ezekiel apunguza Mwili ili kuendana na Mpenzi wake


Staa wa filamu, Aunt Ezekiel aliye katika mapenzi na Dansa Moses Iyobo, ameamua kukimbilia gym kwa ajili ya kupunguza unene unaomuandama ili kulinusuru penzi lake.

Akizungumza na chanzo cha uhakika, Aunt amesema ameanza mazoezi ya nguvu kila asubuhi ili aweze kupunguza mwili aendane na mpenzi wake kwani mwili wake ni mkubwa kuliko wa mwenzie.

“Daah, nimeona nitapoteza penzi langu bure, nimekuwa mnene kumpita baby kitu ambacho siyo sawa, nilikuwa na kilo 87, hivi sasa nimepunguza kilo sita,” alisema.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!