Tuesday, July 19, 2016

Ben Pol Adai kuwa Muziki Umempa Heshima kubwa


Mkali wa muziki wa R&B Bongo, Ben Pol amedai kuwa muziki umempa heshima kubwa kwenye maisha yake kwa kuweza kuisaidia familia yake.

Wimbo wa ‘Moyo Mashine’ wa Ben Pol umezidi kufanya vizuri kwenye Radio na TV kubwa Afrika.Muimbaji huyo ameiambia BBC Radio kuwa kwa sasa muziki umemsaidia kusomesha wadogo zake wawili kwenye shule nzuri.

“Wadogo zangu wapo wawili nimewatoa shule ambazo naona siyo nzuri nimewapeleka shule nzuri wanasoma nina wahudumia kila kitu. Wazazi wangu sasa hivi wameshakuwa watu wazima kidogo ufanisi umepungua mimi ndio nipo responsible,” amesema Ben Pol.

Aidha staa huyo ametoa sababu ya kuupa wimbo wake mpya jina la ‘Moyo Mashine’ ni kutokana na moyo umekuwa ukifanya kazi kubwa kwenye mwili kama mashine.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!