Saturday, July 16, 2016

Faiza Ally aeleza jinsi wasanii wa filamu wa kike wanavyotafuta ‘kiki’ zisizo na faida


Msanii wa filamu Faiza Ally amewataka wasanii wenzake wa filamu kuacha kutafuta ‘kiki’ ambazo haziwanufaishi katika kazi zao.

Faiza amesema wasanii wengi wa kike wa filamu wanatafuta kiki za mapenzi bila kujua kiki hizo zitawasaidiaje.

“Kiki sio mbaya lakini hiyo kiki inakusaidiaje?, mimi ukiona nafanya kiki ujue kuna kazi ambayo inakuja, sio kufanya kiki alafu unakaa kimya ilimradi uonekana na wewe upo, kwa hiyo mimi ningewashauri wasanii wenzangu wa filamu tufanye kazi,” alisema Faiza.

Muigizaji huyo kwa sasa anajipanga kuachia filamu yake mpya iitwayo ‘Baby Mama Drama’.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!