Saturday, July 30, 2016

Freeman Mbowe Aitwa Polisi kwa Mahojiano Jijini Dar


UJUMBE ALIOANDIKA MBOWE KWENYE UKURASA WAKE WA TWITTER

Jana usiku nilipata wito nikitakiwa kwenda Polisi Kanda Maalum Ya Dar es salaam na Zonal Crime Officer Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Wambura, akihitaji nifike leo Jumamosi 30/07/2016, lakini leo nipo Marangu Kilimanjaro kuhudhuria maziko ya Baba yake mzazi Devotha Minja, Mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA.

Na kesho Jumapili 31/07/2016 nitakuwa katika shughuli za kuuaga mwili wa mfanyakazi mwenzetu na aliyekuwa mpiga picha wa Tanzania Daima, Ndugu Joseph Senga aliyefikwa na umauti akiwa kwenye matibabu nchini India , ikiwemo mimi kusafiri kwenda Kwimba Mwanza kwa ajili ya maziko siku ya Jumatatu 01/08/2016.

Najaribu kurekebisha ratiba zangu niweze kwenda Polisi kesho Jumapili 31/07/2016,kwani nimesisitizwa hivyo ingawa sijafahamu naitiwa kitu gani.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!