Friday, July 15, 2016

Gigy Money Akiri Kujiuza lakini Nay si type yake


Gigy Money amedai kuwa lisemwalo lipo kuwa yeye ni msichana anayejiuza, lakini Nay wa Mitego si mwanaume wa type yake.
Wawili hao wamekuwa wakirushiana vijembe tangu Gigy amshutumu Nay kwa kutomlipa ujira wake baada ya kumtumia kama model kwenye video ya wimbo wake, Shika Adabu Yako.

Nay anadai kuwa Gigy hana lolote zaidi ya kujiuza tu mjini.

“Of course inawezekana najiuza lakini wapo wa kuninunua sio type yangu yeye kwasababu dau langu mimi yeye ni kula miaka mitatu,” Gigy alimuambia mtangazaji wa Jembe FM, JJ.

“Kwahiyo sikatai mtu kusema najiuza kuniita malaya au vyovyote. Na kweli mimi najiuza ndio maana yeye akaninunua mara mbili kwenye nyimbo zake sababu I am a video vixen na nipo kwaajili ya hiyo kazi. Kwahiyo najiuza of course ndio maana amefanya na mimi video mbili hajaoni watu wengine?” amehoji.

“Aliniahidi hela kwenye makubaliano ndio hana pesa ya kunilipa, so sishangai kusema najiuza.”

Gigy ameendelea kusisitiza kuwa anamfananisha rapper huyo na muimba mipasho na anaamini kuwa anatafuta ‘kiki’ kupitia kwake!
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!