Wednesday, July 27, 2016

Hatimaye Petitman Arudi kwa Esma Platnumz


Utata uliokuwepo kati ya wapenzi wawili Petitman na mama watoto wake umekwisha baada ya vuta nikuvute ya familia hizo mbili. Mama mzazi wa Petitman amewahi kusikika akisema kuwa hamtaki Esma kuwa mkwe wake kutokana na vitendo vyake.
Pia walakini mwingine wa mapenzi haya ulikuwa mgumu pale Madam Wema Sepetu alipotengana na Diamond Platnumz kipindi kile na kupelekea kukosa ushirikiano kwa kutokea makundi mawili kati ya Petiti na madam na upande wa Diamond Platnumz na mdogo wake Esma

Wadau wengi wanasema kurudiana kati ya Petitman na mdogo wa Diamond ni kwa sababu sasa hivi Petit hayupo tena na Wema kitendo kilichomfanya Esma kurudiana kiurahisi na baba watoto wake kwa kuwa hakukuwa na kipingamizi tena.

Hata hivyo Petitman usiku wa juzi mbele ya camera  na umati wa watu alisema “sioni haja ya kuendelea kuchepuka na wanawake wengine kwa kuwa nimeona kuwa na mademu wengine ni kujipa stress tu, kwa kifupi nimezima simu feki na nimerudiana na mzazi mwenzangu ili tuweze kumlea mweznetu kwa pamoja”.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!