Tuesday, July 12, 2016

Hatimaye Wema Sepetu Amtaja Petit Man Kuwa Ndio Alisababisha Wasanii wa Endless Fame Wasifanye Vizuri


Malkia wa filamu na mkurugenzi wa Endless Fame, Wema Sepetu amefunguka na kueleza sababu ya wasanii wa label hiyo kutofanya vizuri.
Akiongea nasi, Wema amesema mfanyakazi wake Petit Man ndiye aliyosababisha hayo yote kutokea.

“Naweza kusema kuwa kwasababu muda mrefu sana nimemwachia Petit Man akifanya hiyo kazi na sidhani kama alikuwa anaitendea haki kwahiyo ‘let us another six month tusimame sisi kama sisi kwasababu ujue kwenye vitu kama hivi kumtrust mtu labda afanye hiki may be unaweza ukawa unamsapoti afanye any then mwisho wa siku hafanyi unajua kuna vitu vingine vinaingiliana vya kibinaadamu tu,” alisema Wema.

Mirror pamoja na Ally Luna miongoni mwa ya wasanii wa label hiyo.

Hata hivyo Petit Man kwasasa hayupo tena Endless Fame, yupo label ya ‘LFLG’ inayomsimamia Billnas pamoja na Nuh Mziwanda.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!