Saturday, July 30, 2016

Jokate Amwaga Misifa kwa Alikiba


Jokate alitumia ukurasa wake wa Instagram kumwaga sifa hizo na kudai kuwa akiwa amenuna akisikia sauti ya Alikiba anajikuta anafurahi kwani anavutiwa sana na sauti hiyo.

“Alikiba ni King wa kutoa ngoma baada ya ngoma, King asiye kuwa na mbwembwe, ni mzuri kuliko wote, ni mfalme wa sauti ya kumtoa nyoka pangoni. Nikinuna najikuta nafurahi nikisikia sauti yake, hapa nimesikiliza ‘Nisamehe’ nairudia tu, Nisamehe ni wimbo wa taifa unakuja kwa kasi ya ajabu”.Aliandika Jokate

Alikiba na Baraka the Prince wanategemea kuachia wimbo ambao utaiwa ‘Nisamehe’ ni wimbo wa Baraka the Prince ameshirikisha Alikiba.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!