Monday, July 4, 2016

Kilichomfanya Young Dee Kuvuta Bangi ni 'Makundi'


Waswahili husema: “lisemwalo lipo kama halipo laja’. Usemi huu umedhihirika baada ya kuwepo tuhuma siku nyingi kuwa rapa David Genzi maarufu Young D kuwa anatumia dawa za kulevya naye kuzikanusha kila mara.

Hatimaye Young D ameamua kuutua mzigo huo na kukiri kuwa kwa zaidi ya mwaka mmoja amekuwa akitumia dawa za kulevya pamoja na kukiri kilichomwingiza huko.

Kama ulifikiria rapa Young Dee alitumbukia kwa bahati mbaya katika matumizi ya dawa za kulevya, mwenyewe ameiambia Starehe kuwa alifahamu fika kwamba anaingia kwenye unga tofauti na wengine wanapoanza kutumia kwa mara ya kwanza.

Wasanii wengi waliokiri kutumia dawa za kulevya wamekuwa wakitoa ushuhuda kuwa walianza bila kujua. Wengi hueleza kuwa walianza kwa kuwekewa katika bangi au sigara na marafiki, wapenzi au wafanyabiashara.

Young Dee ameyasema hayo wiki moja baada ya kutangaza rasmi mbele ya vyombo vya habari kuwa amekuwa akitumia unga kwa kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kuamua kuacha na kupatiwa matibabu na wanasaikolojia.

Akizungumza mapema wiki iliyopita alisema kitu kilichomvuta kutumia dawa za kulevya ni kundi la marafiki ambalo alikuwa akiambatana nalo kipindi alipolegalega katika kazi zake za muziki.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!