Wednesday, July 27, 2016

Koffi Olomide Ahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela DRC


Mwanamuziki nguli wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Koffi Olomide amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela huko DRC kwa kumpiga teke mmoja wa madansa wake aitwaye Pamela akiwa nchini Kenya.

Nguli huyo wa muziki wa Rhumba amehukumiwa muda mfupi baada ya kukamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa.

Koffi alikana tuhuma za kumpiga dansa huyo na mwanasheria wake aitwaye George Wajackoyah naye amelaani kitendo cha polisi kutumia nguvu kubwa wakati wa kumkamata staa huyo.

Staa huyo alikamatwa nchini Kenya Ijumaa iliyopita na kurudishwa DRC kesho yake asubuhi baada ya video yake kusambaa mitandaoni ikimuonesha akimpiga teke mmoja wa madansa wake aitwaye Pamela mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Jomo Kenyatta (JKIA) kwa ajili ya tamasha.

Koffi anadaiwa kufanya tukio hilo baada ya Pamela kukorofishana na mwanamuziki wake aitwaye Cindy Le Couer anayedaiwa kuwa ni mpenzi wa Koffi.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!