Sunday, July 17, 2016

Linah anakuja na Wimbo Mpya - 'Samaki'


Linah amedai kuwa wimbo mpya anaotaka kuutoa huo utakaoitwa 'Samaki' na ni wimbo ambao ameamua kufanya remix ya wimbo wa Galatone.

Baada ya mengi kuzungumzwa na zilizo chini ni kuwa Linah na Billnass ni wapenzi wa siri na hawataki kuweka wazi mahusiano yao ila kwa sasa mambo yanaweza yakawa wazi kwakua mwanadada Linah ametumegea siri kuwa anakuja na wimbo wake wa samaki.

Linah amesema kwamba wimbo huo utaitwa samaki na ni wimbo ambao ameamua kufanya remix ya wimbo wa Galatone Samaki akiwa amemshirikisha Billnass hivyo mashabiki zake wakae tayari kuupokea.

Hata hivyo Linah hakutaka kuweka wazi suala la mahusiano yake na Billnass kwani aliendelea kusema yeye na Billnass ni washikaji tu na ameamua kumshirikisha kwa kuwa ameona voko zake ndio zitaingia vizuri katika wimbo wake huo.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!