Thursday, July 21, 2016

Lulu Michael Adai Hana Tatizo na Hamisa Mobeto, ni Baada ya Kudaiwa Kumpora Bwana


Msanii wa filamu, Elizabeth Michael aka Lulu amekanusha tetesi za kwamba ana bifu na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Dj Majay, Hamisa Mobeto.
Muigizaji huyo ambaye kwa sasa anadaiwa kutoka kimapenzi na Majay, aliingia kwenye malumbano na baadhi ya mashabiki wa Mobeto katika mitandao ya kijamii wakimtuhumu kuiba bwana.

Akiongea nasi Ijumaa iliyopita, Lulu amesema hata tatizo na Mobeto ambaye ni mama wa mtoto mmoja aliyezaa na Majay.

“Sipendi sana kuongelea issue ambayo nitakuwa kama nachochea, mimi ni mtu fulani very peace, very very peace, sina tatizo naye,” alisema Lulu.

Akiongelea kama ni kweli kuna watu walikuwa wanatumwa na Mobeto ili wamtukane alisema “Siwezi kujua kwa sababu sijafuatwa direct, lakini sina tatizo naye, mtu akinipa kijembe namchukulia kama mtu kanipa kijembe”

Hata hivyo, Lulu na CEO wa EFM, Dj Majay kwa sasa wapo karibu zaidi, kwani wawili hao wamekuwa wakipost picha zao katika mitandao ya kijamii wakiwa pamoja.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!