Wednesday, July 20, 2016

Makahaba Waivamia Dodoma


Wasichana wanaofanya shughuli ya kuuza miili, maarufu kama dada poa( makahaba) wameongezeka katika viunga vya mji wa Dodoma tayari kuvizia wageni watakaohudhuria Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM. 

Wasichana hao, ambao inaaminika wanatoka katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Arusha, Iringa na Mbeya, wameonekana kwenye maeneo mbalimbali ya starehe wakisaka wanaume nyakati za usiku. 

Madada poa ambao kwa kawaida hufurika mjini hapa wakati wa vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano, wamekuwa wakiwatoza wateja hadi Sh30,000 kwa ambaye anataka kulala naye hadi asubuhi. 

“Kama unataka madada poa nenda kwenye baa maarufu za mjini hapa nyakati za usiku. Mwanangu mbona mfuko wako tu. Ukitaka wa kulala naye hadi asubuhi, ukitaka wa saa kazi kwako,” alisema mmoja wa wanaume katika moja ya baa maarufu mjini hapa.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!