Saturday, July 30, 2016

Malaika Asakwa na Freemason


Mwanadada mkali wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wa “nawararua” Malaika ajikuta kwenye mtego wa kuwindwa na Freemason.

Hivi karibuni Malaika amekuwa mmoja kati ya wasanii wanaosadikiwa kujiunga na dini ya Freemason, na akituhumiwa kwamba baadhi ya mambo yanayomzunguka ni ishara au alama za freemason ikiwemo jina lake la Iluminati, mapozi ya picha zake pamoja na namba yake ya simu kuwa na sita sita (666) mwishoni. 

Malaika akiongea na eNewz alisema kwamba “kwa kweli nashindwa kupata jibu sahihi lakini ni kweli nilishafuatwa na watu ambao wapo katika hiyo Freemason, hata hivyo siwezi kulizungumzia zaidi ya hapo, Pia namba yangu ya simu ina 666 na namba sita kwangu inamaana nyingi saana na imebeba maisha yangu pia ”.

“Mwache mtu akuhukumu kutokana na vile anavyotakiwa akuhukumu na once ukitoka tumboni kwa mama yako watu walikuongelea na mpaka unaanza maisha yako wanakuongelea so waache watu wakuzungumzie inakuwa ni vizuri zaidi” aliendelea kusisitiza Malaika.

Alimalizia kwa kusema “Mimi ni mcheshi saana lakini pia mashabiki zangu wategemee kazi nzuri. Yataibuka mambo mengi ya 'ufreemason' lakini tunajaribu tu kutengeneza mziki mzuri na kwa kipindi hiki nimefanya kazi na watu wa nje ya Tanzania.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!