Friday, July 15, 2016

Mama Wema Sepetu Afunguka ya Moyoni kuhusu Mwanae


Mama yake Wema Sepetu, Miriam Sepetu amefunguka kwa kusema anachukizwa na kitendo cha mwanae kupakaziwa habari ya kuwa ana gonjwa la mapenzi.

Akiongea nasi, Mama Wema amesema akiikumbuka kauli hiyo naumia sana moyo.

“Gonjwa la mapenzi ni gonjwa gani?, wewe mwanao uliyemzaa unaweza kumwambia ana gonjwa la mapenzi,” alisema Mama Wema kwa ukali. “Hii kauli imeniumiza sana, watu wake au mashabiki wanaosikia wanatafsiri nini, binafsi hii kauli imeniuza sana,”

Pia Mama Wema amewataka waandishi wa habari kuacha kuandika habari za kumchafua mwanae bila sababu.

Mama Wema ni mmoja kati ya watu wa karibu wa Wema Sepetu ambao walihudhia show ya maklia huyo wa filamu ‘The Black Tie’ iliyofanyika katika ukumbi wa King Solomon weekend iliyopita.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!