Monday, July 18, 2016

Millen Magese Aanza kutafuta Mtoto kwa Njia ya kupandikiza (IVF)


Huenda Miss Tanzania wa zamani, Happiness Millen Magese siku za usoni kama Mungu akipenda akawa na furaha kama ya wanawake wengi duniani – furaha ya kupata mtoto. 

Ni kwasababu tatizo lake la Endometriosis limemuondolea matumaini ya kuwa mama lakini sasa inaonekana kuwa matumaini yamerejea, shukrani kwa sayansi ya IVF. 

 Kwa mujibu wa post aliyoiweka Instagram, huenda Millen akawa amefanyiwa mchakato huo May 13 na hivyo siku za usoni anatarajiwa kuwa mama. 
 
“Sijawa mama tayari lakini ninakikumbatia kila kitukilichoongezwa kwenye mwili wangu na kwenye maisha yangu kwa ujumla tangu May 13,” inasomeka sehemu ya post aliyoiweka inayomuonesha kwenye video akitembea kwa furaha kwenye ufukwe wa bahari==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!