Wednesday, July 13, 2016

Mtoto wa kigogo mbaroni kwa tuhuma za kumbaka denti form one


Justine Ambrose (30) ambaye ni mtoto wa kigogo mmoja wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumbaka denti wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Kigonseram tukio lililotokea Julai 2, mwaka huu.
 
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoani hapa, Zubery Mwombeji alisema lilitokea usiku katika Kijiji cha Kitai muda mfupi baada ya mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 14, kushuka kutoka katika gari lililomtoa kijijini kwao Ngingama, Lituhi akielekea shuleni kwao.

Alisema aliposhuka, mtuhumiwa huyo ambaye pia ni mfanyakazi wa kukusanya ushuru wa Halmashauri ya Mbinga katika geti la Kitai, alimshika kwa nguvu na kumwingiza kwenye kibanda cha walinzi, ambako licha ya kupiga kelele zilizokosa msaada, alimfanyia unyama huo na kumwachia maumivu makali.

Katika wodi maalum ya wagonjwa wanaotibiwa kwa bima ya afya, mwandishi wetu alimshuhudia mtoto huyo akiwa na hali mbaya, huku akizungumza kwa shida.

“Wakati anatumia nguvu ya kunivuta kuelekea kwenye kile kibanda nilikuwa nikipiga kelele, yeye alikuwa akikazana kuniziba mdomo lakini sikupata msaada wowote mpaka alipofanikisha kitendo chake cha kunifanyia unyama huu,” alisema mtoto huyo alipotakiwa kufunguka kuhusu kilichomsibu.

Alisema kutokana na maumivu makali aliyokuwa nayo baada ya kitendo hicho, alishindwa kwenda popote na kulazimika kulala ndani ya kibanda hicho hadi kesho yake ambapo wasamaria wema walimpa msaada wa kumsa risha Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mbinga ambako alipatiwa hati namba tatu ya polisi (PF 3) na kwenda kutibiwa.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mbinga, Elisha Robert alithibitisha juu ya kubakwa kwa denti huyo, lakini alikataa kutoa maelezo zaidi.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!