Wednesday, July 27, 2016

Mwanafunzi wa DUCE Achomwa Kisu Baada ya Kufumaniwa na Mpenzi wake


Ni wanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu UDSM college ya DUCE kilichopo Chang'ombe, ilikua Jumapili ya tarehe 24/7/2016.

Jamaa aliyefahamika kwa jina la Jimmy alimfumania mpenzi wake jina Leah (wanachuo wote) na mwanaume mwingine nyumbani kwa mwanamke baada ya hapo Jimmy akawa mpole na akarudi kwake then yule mwanamke akamfuata huko kwake kwa lengo la kuomba msamaha na ndipo jamaa akamchoma kisu cha tumbo na kumpiga na chupa kichwani

.
Hadi sasa mwanamke yuko hospitali ya Temeke hoi na jamaa yake sasa yuko Chang'ombe kituo cha Polisi.


Jamani mapenzi yapo na wanawake ni wengi zaidi tupende kwa akili sio moyo huyu jamaa atajuta sana kwa uamuzi wake wa kukurupuka.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!