Friday, July 15, 2016

Mwigizaji Shamsa Ford Adaiwa Kuchumbiwa


UBUYU uliokolea rangi jijini ni kwamba staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford anadaiwa kuchumbiwa na mfanyabiashara maarufu Bongo, Chid Mapenzi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na mwanaume huyo kilieleza kuwa, wawili hao wapo kwenye mipango lukuki ya kufunga pingu za maisha na mwanzoni mwa wiki hii Chid alifunga safari hadi ukweni mkoani Dodoma kutoa mahari ambayo haikufahamika ni kiasi gani cha fedha.

Baada ya kuunasa ubuyu huo, shushushu wetu alitafuta ‘kontakti’ za msanii huyo aliyewahi kujizolea umaarufu na Filamu ya Chausiku, alipoulizwa alionesha mshktuko na kuangua kicheko;

 “Khaa! Huo ubuyu kiboko, hakuna kitu kama hicho jamani, mimi yule ni mtu wangu wa karibu tu isitoshe kwetu siyo Dodoma, watu bwana!”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!