Saturday, July 16, 2016

Nape: Ukinunua CD isiyo na stika, wewe ni mwizi kama wezi wengine na utashughulikiwa


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye baada ya kufanya ziara Ijumaa hii katika maeneo ya Kariakoo kukagua na kukamata CD ambazo hazina stika ya TRA, amewataka watanzania kuacha tabia ya kukunua CD ambazo hazina stika za TRA.

Akiongea na waandishi wa Habari katika msako huyo, Nape amesema yeyote anayekamatwa na CD ambao haina stika ya TRA atashtakiwa kwa kosa la kuhujumu uchumi.

“Kila anayenunua sasa kazi ya sanaa ambayo haina stika ya TRA naye ni mwizi kwa kama mwizi yoyote sababu ameshirikiana na muuzaji ambaye hajalipa kodi, hata tukikukuta na CD moja haina stika wewe ni mwizi kama mwizi mwingine tutashughulika na wewe,” alisema Nape.

Katika ziara hiyo zaidia ya maduka 40 yamefungwa huku CD fake zikichukuliwa kwa ajili ya kuaribiwa.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!