Saturday, July 16, 2016

Nay wa Mitego ahojiwa na polisi kwa masaa, aachiwa kwa dhamana


Msanii wa muziki wa Hip Hop, Ney wa Mitego amehojiwa kituo cha Polisi Kati na kupewa dhamana kufuatia tuhuma zinazomkabili.

Kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema msanii huyo alihojiwa juzi kituoni hapo na yupo nje kwa dhamana, huku jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tuhuma zinazomkabili.

“Ni kweli juzi mchana tulimhoji Ney wa Mitego na yupo nje kwa dhamana kuhusu kukamatwa kwake nitatoa taarifa kwa nini tulimkamata,”amesema Kamanda Sirro.

Hata hivyo, Bongo5 imejaribu kumtafuta rapper huyo wa wimbo ‘Pale Kati Patamu’ bila mafanikio, kwani kila akipigiwa kupitia simu yake ya mkononi haipatikani.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!