Friday, July 29, 2016

Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) Dkt. James Munanka Wanyancha.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi iliyotolewa jana Mjini Dodoma imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia jana tarehe 28 Julai, 2016.

Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Joseph Odo Haule kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Barabara.

Uteuzi wa Bw. Joseph Odo Haule umeanza jana tarehe 28 Julai, 2016.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Joseph Odo Haule alikuwa Meneja wa Mfuko wa Barabara (Road Fund).

Wajumbe wengine wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wanaendelea katika nafasi zao.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!