Friday, July 15, 2016

Roma na Kala Jeremiah wamtembelea Lowassa


Rapa kala Jeremiah na Roma Mkatolikia walikuwa wakichota busar za Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa walipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa wasanii hao, walifanya mazungumzo na Lowassa ingawa hawakueleza walichozungumza na mwanasiasa huyo mkongwe aliyegombea urais mwaka jana kwa tiketi ya Chadema akiungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa.

“VIJANA WANAPOKUTANA NA MZEE. #MUNGU IBARIKI TANZANIA,” aliandika Kala Jeremiah kwenye picha waliopoz na Lowassa. Naye Roma Mkatoliki  amepost picha na kuandika #DoneTheMeeting With Hon. #E_LOWASA. 

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!