Sunday, July 31, 2016

Sallam atoa hint ya ujio wa album mpya ya Diamond


Kuna uwezekano mkubwa kuwa Diamond anajiandaa kuachia album yake mpya. Meneja wa staa huyo ambaye kwa sasa yupo Afrika Kusini ametupa hint kuwa santuri mpya ya msanii wake ipo njiani kuja. Sallam Sharaff amepost picha hiyo chini na kuandika kwa maneno yanayotafsiriwa kwa Kiswahili ‘hii ni tarehe sahihi ya kuachia album.’

 Kwa sasa muimbaji huyo anafanya vizuri na wimbo wake Kidogo aliowashirikisha P-Square. Video ya wimbo huo hadi sasa ina zaidi ya views milioni 2.2 kwenye Youtube.


==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!