Friday, July 1, 2016

Shilole kutafuta Mume Igunga


MKALI wa Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amejutia kuwapenda wanaume wa mjini kuwa ni wavivu kila sekta hivyo anajipanga kwenda kijijini kwao Igunga,Tabora kutafuta mume.
Akistorisha na Showbiz Xtra, Shilole alisema kuwa, hataki tena kujichosha akili kwa wanaume wa mjini kwa vile ni wavivu bora aende Igunga kumpata mwanaume atakayeweza kufanya kazi kutokana na vyakula asili anavyokula.

“Wanaume wa mjini wamezoea chipsi mayai, hawawezi chochote bora wa kijijini wanakula dona na wana akili za kufikiria,” alisema Shilole.

Shilole alikuwa akitoka kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!