Sunday, July 10, 2016

Waziri Mkuu wa India awasili nchini kwa ziara ya siku mbili


Tanzania imeendelea kuwa na neema ya kutembelewa na viongozi wa mataifa mengine baada ya usiku wa kuamkia leo Jumapili Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi  kuwasili nchini ambapo alipokelewa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na viongozi wengine wa kitaifa na kimkoa Jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akisalimiana na Mhe. Modi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!