Friday, July 15, 2016

Young Killer Atamani kujiunga na lebo ya WCB


Hivi karibuni kulikuwa na tetesi za kuwa huenda Young Killer atakuwa miongoni mwa wasanii atakayeungana na timu ya WCB.

Sasa July 14, 2016 chanzo chetu kilimpata Young Killer na kueleza tetesi hizo na kusema..‘Hizo taarifa si za kweli maana watanzania wanakuambia tuletee picha halafu wao watapata maneno ya kuandika hii ilitokana na ile picha niliyopiga na Diamond Platnumz kipindi nilivyoenda ofisini kwake, lakini siko kwenye lebo ile ile ikitokea naingia natamani kufika mbali kimuziki’- Young Killer


==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!