Wednesday, July 13, 2016

Zari na Diamond watuma ujumbe kuwa mambo ni shwari licha ya kuwepo tetesi za mgogoro wa familia


Kuna tetesi nyingi sana zimevuma kwenye mitandao ya kijamii wiki hii kuhusiana na Diamond na Zari. Miongoni mwa tetesi hizo ni pamoja na kuwa Zari haelewani kabisa na ndugu zake Diamond akiwemo mama mkwe wake na wifi yake, Esma.

Hilo Zari alilielezea kwa mafumbo kwenye Snaochat na kudai kuwa hajali kama nchini au ukoo usipomkubali, ilimradi tu wanapendana na mpenzi wake.
 
Tetesi nyingine ni kuwa staa huyo wa ‘Utanipenda’ si mwaminifu kwenye uhusiano wao na kwamba huenda akawa na ukaribu usio wa kawaida na Hamisa Mobetto.

Yote hayo yanaonesha kuwa si kitu kwenye couple hii na wameamua kuonesha kuwa wapo strong kupitia Instagram. Wamepost picha na video kadhaa wakiwa na mtoto wao Tiffah kuashiria kuwa mambo ni shwari.

“Sending love from the other side from me and mines. Have a blessed week,” ameandika Zari kwenye post moja wapo.

Naye Diamond akiwa na familia yake hiyo ameandika, “Aint nothing better than spending time with the people that you love from the bottom of your heart……hata ukiwa kijuso, ukiwa nao kasura kanakuwaga kama kanapata Uhendisamu kwa mbaaaali kwa furaha.”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!