Friday, July 15, 2016

Zitto Kabwe Atoa Kauli baada ya kutumbuliwa kwa kada wa ACT Wazalendo (aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya Tarime)


Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo na Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Zuberi Kabwe amemshukia Rais Magufuli baada ya kada wa chama hicho kutumbuliwa siku chache baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Tarime.

Hidaya Usanga ambaye ni kada wa ACT Wazalendo alikuwa pia mgombea ubunge katika jimbo la Malinyi mkoani Morogoro, uteuzi wake ulitenguliwa mara moja na Rais Magufuli kwa kile kilichoelezwa kuwa ni sababu za kichama.


Zitto Kabwe amehoji kauli ambazo Rais Magufuli huwa akizinadi mara kwa mara kuwa anachagua watendaji wa serikali kuangalia uchapakazi na si uchama sasa kwanini Hidaya ameondolewa katika nafasi hiyo?

Rais Magufuli amekuwa akisema kuwa maendeleo hayana chama na kuwa sote tunawajibu wa kushirikiana bila kujali chama wala dini wala kabila, lakini leo Rais anamtumbua mtu kwa sababu si kada wa CCM, hii inaonyesha kuwa anayoyazungumza Rais Magufuli hayaamini, alisema Zitto Kabwe.

Zitto alihoji sababu ya nafasi za utendaj serikali kupewa makada wa CCM, na alieleza Ikulu hawapo makini katika teuzi wanazozifanya kwani hii si mara ya kwanza hizi teua, tumbua zinatokea na kuwa tangu kwenye uteuzi wa wakuu wa wilaya, mikorogo imekuwa mingi.

Hadi sasa hakuna taarifa rasmi kutoka Ikulu kuhusu kutenguliwa huko kwa Hidaya Usanga.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!