Tuesday, August 23, 2016

Diamond na Alikiba kushindania ‘Best Male Artist in Eastern Africa’ tuzo za Afrima 2016

Diamond Platnumz na Alikiba watachuana mwaka huu kuwania kipengele cha Best Male Eastern Africa kwenye tuzo za All Africa Music [Awards] 2016 za nchini Nigeria.

Waandaji wa tuzo hizo wametoa orodha ya kwanza ya wasanii wanaowania mwaka huu.Diamond na Kiba wana upinzani pia kutoka kwa Bebe Cool, Eddy Kenzo, Jose Chameleone na Navio wa Uganda. 

Hata hivyo hakuna msanii wa Tanzania aliyetajwa kwenye kipengele hicho upande wa wanawake.Tuzo hizo zitatolewa mwezi November jijini Lagos, Nigeria.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!