Tuesday, August 9, 2016

Mtoto Aliyewekewa Betri Kwenye Moyo Kuruhusiwa Kupita Kwenye Viwanja vya Ndege Bila Kukaguliwa na Mashine

Kadi ya kumtambulisha mtoto Happiness John (5) kimataifa baada ya kufanyiwa upasuaji na kuwekewa betri ndani ya moyo inatengenezwa nchini Afrika Kusini. Happiness ambaye alifanyiwa upasuaji huo Julai 15 na kuruhusiwa kutoka hospitalini wiki moja iliyopita, anatakiwa kuwa na kadi tambulisho ambayo itamuwezesha kutofanyiwa ukaguzi wa kielektroniki. Kwa sasa mtoto huyo amepewa kadi ya muda ambayo inamruhusu kutopita katika maeneo yenye mionzi kwa ajili ya ukaguzi, ikiwamo viwanja vya ndege na majengo yenye ulinzi mkali.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!