Tuesday, August 23, 2016

Raymond Azawadiwa gari jipya na WCB kwenye birthday yake

Uongozi wa WCB umeendelea kumwaga zawadi ya magari kwa wasanii wake na sasa bahati imemuangukia Raymond.
Jana ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa msanii Raymond, uongozi wa WCB ukaamua kumfanyia sherehe msanii wao huyo kwenye ikulu ya Diamond iliyopo huko Madale lakini kubwa zaidi ni zawadi ya gari aliyopewa kwenye sherehe hiyo. Bosi wake, Diamond, ameweka kipande cha video kinachoonesha msanii huyo akikabidhiwa gari hilo aina ya Rav4 yenye rangi nyeusi.

Raymond anakuwa msanii wa pili kutoka WCB kukabidhiwa gari na uongozi huo baada ya mwezi Mei mwaka huu uongozi huo kumkabidhi Harmonize gari aina ya Mark X yenye rangi nyeusi. Rangi nyeusi imeonekana kutawala WCB kwani hata Diamond anamiliki BMW X6 yenye rangi nyeusi pia.

Wamebakia wasanii wawili ndani ya kundi hilo ambao bado hawajakabidhiwa magari swali, je ni nani atakuwa wakwanza kuipata zawadi hiyo kati ya Queen Darlin na Rich Mavoko?
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!