Wednesday, August 31, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 33 & 34 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )


Mtunzi:EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA....

“Duu kweli malipo ni hapa hapa duniani?”
“Kwa nini baba?”
“MAMA YAKO NI KATILI SANA TENA ZAIDI YA SANA JAPO USONI MWEKE NI MWAMA KUPITILIZA”

Maneno ya baba yakanicha mdomo wazi huku nikishangaa nisijue ni kwanini amesema mama yangu ni katili sana

ENDELEA...
Nikaendelea kumtazama baba kwa macho ya mshangao
“Mama yako ni katili sana kiasi kwamba aliyaaribu maisha yangu kwa kiasi kikuwa....Kipindi ambacho wewe bado hujazaliwa tulikuwa tunapendana sana na kaka yangu na kwajinsi tulivyokuwa tunapenda tuliamini kwamba hakuna kitu amaco kitaweza kutuchonganisha...Ila ninanakumbuka kipindi baba yaka anaingia jeshini mimi nilifeli majaribio kutokana kipindi kile nilikuwa ninaumwa na ugonjwa wa miguu”

“Basi baba yako akaja kukutana na mama yako na kutokana kipindi kile sisi tulikuwa ni fukara sana na wazazi wetu walisha fariki ikabidi kaka ambaye nilisha zoea kumuita kurwa aliniomba nihamie kwa mama yako amaye kwa kipindi kile alikuwa ni daktari ila kwao walikuwa ni matajiri sana kwahiyo swala la pesa kwake lilikuwa ni la kawaida......

Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1991 ambapo mama yako alianza kujiingiza kwenye mambo ya vyama kwa maana uchaguzi ulikuwa unaelekea miaka ya mbeleni.....Mambo mengi sana akawa ananishirikisha kama mtu wake wa karibu sana kiasi kwamba ikafikia kipindi tukaanza mahusianao ya kimapenzi pasipo kurwa kujua na yeye kwa kipindi kile ilikuwa ni ngumu sana kuweza kujua ukweli kutokana alikuwa yupo kambini kwenye kambi ya jeshi Morogoro na sisi tulikuwa tunaishi Dar es Saalam”

“Kuseme kweli mama yako alimpenda sana kurwa na mimi alinichukulia kama kituliza nafsi.....Ninazungumza ukweli ili uweze kumjua mama yako vizuri na yale yote aliyo nitendea”
Nikabaki kimya huku nikiendelea kumsikiliza baba hata mat yenyewe mdomoni hayakuweza kupita sikujua ni kwanini.

“Basi kipindi alipo gundua amepeta mimba yako na ilipo kuwa na wiki mbili akaanza kutengeneza chuki juu yangu na kipindi kile kwa Tanzania masimu yetu yalikuwa ni yale ya mezani hazikuwepo kama hizi za siku hizi,Alipiga simu kambini na kumuomba kaka kuja nyumbani.Basi baada ya kaka kuja akaanza kuniumiza moyo kwa kufanya mambo yao hadharani huku mimi nikiwashuhudia.......Kitendo cha mama yako kutuchanganya kiliniuma sana na nikaapia ipo siku nitamwambia Kurwa kila kitu kinacho endelea ila kitu ambacho ninakijutia hadi leo ni kwajinsi nilivyo anza kumuambia mama yako kwamba nitamwambia kurwa ukweli wote wa mambo tuliyo yafanya na kipindi hicho tayari ujauzio wake ulisha anza kukua”

“Kitu alicho anza kukifanya mama yako ni kuanza kufanya vitisho vya kutaka kuniua na akaniomba niweze kuondoka Tanzania kama maisha yangu ninayapenda.....Ila kutokana alikuwa na damu yangu tumboni nikawa ninavuta subra niweze kumuona mwanangu amabaye ni wewe....na nililikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwengine ambaye alikuwa amenihifadhi na baada ya mama yako kutambua kuwa ninamwanamke mwengine akatua matu na wakatuvamia sehemu ambayo sisi tunaishi na yule mwanamke....Wa...walimuua kwa kumuingiza chupa sehemu zake za siri na kumkata maziwa na kitendo hicho kilifanyika mbele yangu”

Baba akatulia kimya huku machozi yakianza kububujika kiasi kwamba na mimi kwa mbali machozi yakaanza kunilenga lenga.

“Na mbaya zaidi yule mwanamke alikuwa na ujauzito wangu wa mwezi mmoja na nusu na akafariki na mwanangu tumboni na mimi wakanichoma sindano ya sumu kiasi kwamba sehemu hii yote ya chini ya mwili wangu ikawa haifanyi kazi,pamoja na kinywa changu kikawa kimepinda kwa na sikuweza kuzungumza kitu cha aina yoyote...Basi ninakumbuka kuna daktari wa kizungu alikuwa ni rafiki yangu sana aliweza kunisaidi na kwake kulikuwa ni huku Africa kusini....basi nilipo muelezea kuhusiana na yaliyo nikuta akaamu kunileta kuhu Afrika kusini ambapo nilifanyiwa upasuaji na ikawalazimu kunikata miguu  yote miwili na kutokana yule mzee alikuwa na pesa sana akaamua kunichongeshea miguu ya bandia ambayo ni kama hii unayo iona”

Baba akanifunulia suruali yake na kuiona miguu yake ya chuma ikifanana kama ya mwanariadha maarufu Afrika kusini ambaye naye ana miguu ya namna hii,machozi yakaanza kunimwagika huku yakiambatana na maumivu makali ya moyo.

“Basi nilianza kufanya kazi kwa yule mzee na kipindi anafariki hakuwa na mtoto wala ndugu na mali zake zote aliniridhisha mimi na ndio maana unaniona nina mali nyingi kiasi hichi.....Hayo nileyo kueleza ni machache ila kuna mengi sana ambayo mama yako alinifanyia ila kutaoka upo hapa nitakuwa ninakuadisia kila muda utakavyo kuwa unakwenda”

Baba akatoa kitambaa mfukoni mwake na kunipatia na kuanza kujifuta machozi ambayo yananimwagika na nikabaki nikiwa sina cha kuzungumza kwani sikuweza kuamini kama mama anaweza kumfanyia ukatili mtu aliye mbebea damu yake tumboni.Baba akasimam na kuisogelea meze iliyo jaa mizinga ya pombe kali kisha akachukua mzinga mmoja na akamimina kiasi cha kidogo cha pombe kwenye glasi kisha akapiga fumba moja la pombe hiyo huku akiikunja sura yake akionekana kuwa kitu anacho kinywa ni kikali sana kisha akaviweka mezani na kurudi sehemu aliyokuwa amekaa kisha akashusha pumzi nyingi

“Eddy nilikutafuta sana mwanangu kupitia sehemu mbali mbali hususani mitandano ya kijamii ila kitu ambacho kilikuwa ni kigumu ni kuto kulifahamu jina lako.”

Nikaanza kuyaamini maneno ya baba kuwa mama anaroho mbaya kutokana na jinsi alivyokuwa akimkataa Manka na kutaka kumsweka gerezani kwa kunipiga risasa na kitu kingine nilicho kikumbuka ni maneno ya yule dereva taksi ambaye nilipata naye ajali.

“Haaa huyu mama naye yupo.....Kweli Mungu hapendi dhambi kuna siku bwana alikuwa na dereva wake sasa kwa bahati mbaya nikamchomekea kwa mbele ile barabara ya kuingilia K.C.M.C nilikuwa namuwahisha mgonjwa hospitalini.Ahaaaa alikwenda kunilaza polisi hadi siku anaondoka Arusha ndio wakaniachia......Tena hao watekaji kama wanajua wamfanye wa kwanza kufa kwa maana yule mama roho mbaya sana”

Baba akanisogelea na kunishika bega na kuniomba ninyanyuke kisha akaniweka vizuri shati langu na kuniomba twende nje.Akaanza kunitembeza kwenye eneo la jumba lake la kifahari na kwaharaka haraka utajiri wa baba ni mara tano ya utaji alio nao mama.Ila moyoni mwangu sikuweza kuiruhusu chuki iliyopo kati ya wazazi wangu kunitawala moyoni mwangu ila chuki yangu kwa sasa ilibaki kwa baba mkubwa ambaye amemtekana mama akisaidia na Emmy mwanamke aliye jitambulisha kama daktari.

Baba akanionyesha chumba changu kikubwa ambacho nitakitumia kwa kulala na nikikubwa sana na kina vitu vingi sana vya kuvutia japo kwa mama ni tajiri ila baba amezidi kuwa na utajiri mkubwa.Muda wa usiku wageni ambao ni rafiki wa baba wakaanza kukusanyika kwa ajili ya sherehe na kabla ya sherehe kuanza nikawa nipo kwenye chumba maalumu huku nikiwa na mwana mitindo ambaye amenitengenezea suti nzuri inayo endana na mimi na kazi hii ameifanya ndani ya msaa machache jambo ambalo limenishangaza na hapa nikagundua kuwa wezetu wenye nchi zilizo piga hatua wamechangamka sana kwenye utendaji wao wa kazi

“Unajionaje kijana?”
Mwanmitindo aliniuliza baada yakuivaa suti aliyo nitengenezea huku nikiwa nimesimama mbele ya kioo nikiwa nimependeza kiasi kwamba hata mimi kimoyo moyo nikaanza kujisifia kabla sijasifiwa
“Imenikaa vizuri?”
“Hakuna sehemu ambayo inakupa shida kwenye kutembea au imekubana sehemu?”
“Sina kila sehemu imekaa sawa”
“Hembu tembea hadi pale mbele”

Nikapiga hataa kama sita kisha akaniomba nigeuke na kurudi sehemu niliyo simama awali na hadi ninafika nikasikia makofi yakipigwa na nikageuka na kukutana na mama mke wa baba kwa sasa akiingia kwa mwendo wa madaha hadi sehemu niliyo simama

“Unaonekena ni kijana mzuri..mtanashati eheee?”
Sikumjibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kumtazama jinsi anavyo niangalia kuanzia chini hadi juu kwa macho ya dharau

“Josh ninakuomba utoke na tunataka tuzungumze”
Mwanamitindo akatoka na kutuacha tukiwa tumetazamana na mke wa baba na baada ya mlango kufungwa sura yake ikabadilika na ikakusanya mikunjo migi ya hasira.
“Huwezi kuichukua nafasi ya mwangu mbele ya baba yako,sijui amekuokota amekununua,amekuiba ila nitahakikisha hapati chochote kwenye uridhi huu wa baba yako”

Mke wa baba alizungumza huku sura yake akiwa ameikunja na meno yake akiwa ameyang’ata kwa hasira
“Sikiliza wewe mwanamke hunijui sikujui sasa kama unaitaji kunijua utanijua kwa herufi kubwa sawa?”

“Hahaa sina haja ya kukujua omba omba kama wewe usiye na wazazi na nikawaida yenu vijana masikini kama nyinyi hapa Afrika kusini kuwaparamia watu wenye fedha zao na kuwaona ni kama wazazi wenu sasa kama umtumwa na huyo mama yako Malaya aliye shindwa kukulea basi kamwambie nafasi imkwisha”
Nikamtazama kwa hasira mke wa baba kiasi kwamba mwili mzima ukaanza kunitetemeka,
“Na kingine nitahakikisha humalizi wiki utakuwa umeondoka ndani ya hii nyumba”
“Etiii ehee....?”

“Na hakuna cha Etii ehee mbwa wewe uliye kosa pa kula”
Nikajikuta nikiunyanyu mkono wangu wa kulia kwa kasi ya ajabu nikaupeleka kwenye shavu la mke wa baba na kabla haumfikia mlango ukafunguliwa na nikamuona baba akiingia na nikaushusha chini kwa haraka na kumstukia mke wa baba akiangua kiliao huku akilishika shavu lake akidai nimepiga kitendo kilicho zidi kunipandisha hasira

“Mume wangu umeamua kuniletea mwanao aje kuniadhiu mimi....Si ndio?”
Mke wa baba alizungumza kwa sauti ya kufoka na kumuona baba akiwa amenywea na taratibu akaanza kupiga hatau za kumfwata mke wake
“Pole mke wangu.....Eddy mwangu mbona upo hivyo?”
“Yaani mbele yangu unamuita huyo ngedere wako mwanao....?”

“Mke wangu huyo sio ngedere ni mwangangu”
“Wewe vipi kati ya watoto huyo unaweza kusema ni mtoto hembu muangalie anaonekana hivi hivi ni mama yake ni mbwa koko”

Maneno machafu ya mke wa baba yakanizidi kunikasirisha hadi nikashindwa kuizuia hasira yangu na kwaharaka nikamchomoa mikononi mwa baba ambaye anaonekana kuwa anamdekeza mwanamke wake.Nikamvuta karibu ya sura yangu huku nikiwa nimelishika sehemu ya kifuani kwake kwenye gauni lake alilo livaa na nikamuona anayafumba macho yake kwa kuongopa
“Nitakuua”

Nilizungumza kwa hasira na kumsukumia sehemu aliyoo baba na akamdaka mke wake na wote wakajikuta wakianguka chini kisha mke wake akasimama haraka
“Niue sasa kama unaweza”

Nikapiga hataa za haraka hadi sehemu aliyo simama na nikamtisha kama ninampiga kofi akaikuja mikono yake akiuficha uso wake na kwakutuma mguu wangu wa kulia nikipiga teke miguu yake yote miwili na kumrusha juu kidogo kimo cha mbuzi na akaanguka chini kama mzigo na kuendelea kulia,nikapiga goti kwa haraka na kuishika shingo yake na kwa haraka na kumsogelea karibu

“Usidhubutu siku hata moja kumuambia mama yangu ni Malaya na usinifananishe na mnyamwa wa aina yoyote na kama unataka kunifananisha nifananishe na shetani”
“Eddy mwanangu ninakuomba utulize jazba msamehe bure tuu”

Nikaisikia sauti ya baba ikizungumza kwa upole na unyenyekevu  na nikamuachia na kusimama na kumaacha akikohoa kohoa
“Baba kumbe haya ndio maisha unayo ishi na huyu mwanamke asiye na adamu....anakazi ya kukupelekesha kama boya.Wewe ni mwanaume unatakiwa kumtawala mwanamke na si mwanamke kukutawala wewe”

“Mwanangu usizungumze hivyo”
Baba alizungumza huku akiinama na kutaka kumpa mke wake mkono ili amnyanyue na kwa haraka nikaiwahi mikono yao na kuichanisha

“Muache anyanyuke mwenyewe na tuone sasa kama atashindwa kunyanyuka”
Nikamsogeza baba mbali na mke wake ambaye akanyanyuka taratibu huku sura yake ikiwa imejaa machozi na aibu na akawa ananitazama kwa macho wiziwizi na akaanza kupiga hatua za haraka kuelekea mlango ulipo na kabla hajaufikia nikamuita kwa sauti ya ukali na akasimama na nikamfwata hadi sehemu alipo simama.

“Kinacho kuliza ni nini?”
“Mmmm hakuna kitu”
“Futa machozi”
Mke wa baba akaanza kufuta mchozi kwa kutumia gauni leke kisha akabaki akinitazama ninavyo hisi hakuamini kama mimi ninaweza kufanya nilicho mfanyia mbele ya mume wake
“Nenda kajiandae na kwenye sherehe ninakuhitaji nikuone na nitakaa na wewe”
“Sawa”

Mke wa baba akatoka na kuufunga mlango kwa nguvu na kunifanya nianze kucheka na baba naye akanifwatia kwa kucheka
“Baba hivi huyu mke wako unaishi naye vipi?”
“Wee acha tuu mwanangu,Afadhali umekuja na wewe kwa maana huyu mwanamke ananipelekesha sana yaani hadi ikifikia kipindi nikirudi nyumbani tuu furaha yote inanipotea”

“Sasa kwanini na wewe baba unakuwa hivyo?”
“Yaani hata mimi mwenye sielewi ni kwa nini yaani akizungumza yeye huwa mimi sina la kubisha kwake”
“Kwani umeomtoa wapi?”
“Ahaa naye ana historia yeke ndefu tuu nitakusimulia siku nyingine...sasa hivi twende kwenye sherehe nahisi imesha anza na wanatusubiria sisi”
“Sawa baba”

Tukatoka na baba chumbani na kukuta mwana mitindo mlangoni na baada ya kuniona anakisimamisha na kuanza kuiziweka nguo zangu vizuri kisha akatoa viatu vinavyoendana na suti niliyo ivaa ambayo ni ya rangi ya bluu na nikavua viatu nilivyo vivaa na kuvaa alivyo nipa kisha tukaelekea sehemu yenye bustani iliyo pambwa vizuri na kukutana na watu wachache ila wamevali vizuri.Tukakaa sehemu ambayo tumeandaliwa na muongoza sherehe akaendelea na kazi yake,Macho yangu yakawa na kazi ya kutafuta ni wapi alipo mke wa baba na nikamuaga baba ninaelekea msalani(chooni) na akamuomba mlinzi wake mmoja kunifikisha msalani

Nikapita kwenye moja ya kordo na kumuona mke wa baba akiwa amekumbatiana na jamaa mmoja  huku wakiwa wananyonyana midomo yao,mlinzi naye akashuhudia tukio hilo na nikataka kwenda ila jamaa akanizuia na kuitoa simu yake mfukoni na kupiga picha kadhaa na tukaendelea na safari yetu huku moyoni mwangu nikizidi kupata maumivu nikijiuliza ni kwanini baba anaishi na mwanamke wa namna hii

Nikamaliza haya zangu na tukarudi kwenye bustani na hatukuwaoa kwenye eneo walilo kuwepo,Nikamkuta mke wa bab akiwa amekaa pembeni ya baba huku akicheka akimtazama mchakeshaji anaye endelea kufanya yake.Nikajikausha huku mara kwa mara nikimtazama kwa macho makali na nikazidi kuumia pale anavyo mbusu busu baba machavuni na mdomoni akijifanya kama anampenda sana baba

Wakati wa kutambulishwa ukawadia na baba akanitambulisha kama mimi ndio mridhi wake wa pekee kitendo kilicho mchukiza mke wake japo kila nilipo mtazama akatabasamu akiashiria kuwa anafuaha moyoni mwake.Sherehe ikaisha huku moyoni mwangu nikitamani kumuambia baba juu ya tukio alilo lifanya mkewe ila nikaona hatomfanya kitiu chochote.Nikaelekea chumbani kwangu na nikaoga na kupanda kitandani na mawazo ya wapi alipo mama yakanza kunitawala kichani kwangu

Nikanyanyuka na kuisogelea meza iliyo na kumputer aina ya HP,nikaiwasha na kwabahati nzuri nikakuta imeunganishwa na hudumu ya internet.Nikaingia kwenye mtandao unao husiana na taarifa za serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Nikaanza kutafuta tafuta habari itakayo husiana na mama na nikakutana na habari ya iliyo andikwa kwa maandishi makubwa ikisema
“WAZIRI WA AFYA ATOROSHWA HOSPITALINI HUKO AFRIKA KUSINI ALIPOKUWA AMELEZWA”
Nikaanchana nayo kwani ni habari iliyo tolewa mwezi na nusu ulio pita na nikakutana na taarifa nyingine inayo husiana na mama.

{“BI MAGRET INASADIKIKA AMETEKWA NA KUNDI LA KIGAIDI LA AL-SHABABI”}
Mapigo ya moyo yakaanza kuniende mbio na nikaifungua taaribu hiyo na kuanza kuisoma huku mwili mzima ukinitetemeka hadi nijajikuta ninacho kisoma sikilewi.

{“Mume wa Bi Magreti bwana Godwin amabeye ni mkuu wa jeshi kikosi maalumu amedai kuwa mke wake ametekwa na magaidi hao ambao wanahitaji kiasi cha dola za kimarekani milioni 50 kutoka kwenye serikali ya Tanzania ili kumuachia huru waziri huyo”}

{”Raisi aishutumu serilakali ya Afrika kuwa hawapo makini katika swala la ulinzi viongozi wanao toka nchi mbalimbali wanao lazwa kwa ajili ya matibabu katika hospitali zao”}

Nikajikuta nikijikuna kichwa kiasi kwamba nikahisi nywele nitazitoa kwa kuzivuta.Moyo kwa moja nilajua kuwa mama hajatekwa na kundi hilo la magaidi kama inavyo semekana na moja kwa moja atakuwa ni baba ambaye kwa sasa anajifanya kuwa watekaji ni kundi la Al-shababi.Nikaendelea kutafuta habai nyingine na kukutana na habari nyingine ikesema

{“HIZI NDIZO PICHA ZINAZO MUONYESHA WAZIRI BI MAGRET AKIWA MIKONONI MWA MAGAIDI WALIO TOA SIKU KUMI NA TANO KWA SETIKALI YA TANZANIA”}

Nikaanza kutazama picha moja baada ya nyengine na kumuona jinsi mama alivyo fungwa kitambaa cheusi machoni mwake huku kichwani mwake akiwa amewekewa mitutu kama sita ya bunduki aina ya SMG.Machozi yakaanza kunimwagika baada ya kuiona picha nyingine ya mama akiwa amechorwa maandishi ya kiarabu yenye rangi nyekundu kwenye kifufua chake huku mkono mmoja wa mtu ulio valia gloves nyeusi ukimshika kwenye sehemu ya chini ya kidevu chake huku akimminya mashavu yake kwa nguvu.

Nikajikuta mkono wangu ukielekea kwenye kitufe cha kuzimia computer na kurudi kitandani huku machozi yakinimwagika na hasira ikawa imenikaba kifuani mwangu hadi nikahisi kifua changu kinaweza kunipasuka.Sikupata usingizi hadi asubuhi na kitu cha kwanza nikamsubiria baba ili nimpe taaria hiyo.

Baba akanikuta nimekaa sebleni nikiwa nimeshika tama na baada ya salamu nikamuomba nizungumze naye na akakubali na akakaa pembeni yangu na nikanza kumsimulia kuanzai A hadi Z kwa hali aliyo kuwa nayo mama
“Sasa hapo tutafanyaje mwanangu?”
“Una hizo milioni 50?”
“Mmmm hicho ni kiasi kikuwa cha pesa japo ninacho ila ngoja kwanza tujua hiyo hali itakwenda vipi?”

“Basi inanibidi nirudi Tanzania leo?”
“Kwa leo mwangu siwezi kukuruhusu kurudi Tanzania ila ngoja nitwapa hiyo kazi wafanya kazi wangu hiyo kazi”
“Wataiweza kweli?”
“Ndio ila sio hawa una waona hapa kuna wengine nitawapa”
“Lini utawapa?”
“Leo ngoja tupate kifungua kinywa kisha tutakwenda kwa hao watu wangu na sipendi waje hapa kwani wanatafutwa sana kwa matukio wanayo yafanya inanibidi tuwafwate”
“Sawa”

Tukapata kifungua kinywa kisha nika tukajiandaa kwa ajili ya kwenda alipo ndiambia baba na tukatumia gari jengine ambao linaendesha na yule mlinzi wake wa jana sukiku,Ndani ya gari sote tukawa kimya huku akili yangu ikiwa inamuwazia mama yangu.Tukafika kwenye gorofa moja na baba akashuka

“Eddy nisubirini nikaongee na kiongozi mmoja hapa wa jeshi kisha tutawafwata hao watu”
“Sawa baba ila nina ombi”
“Ombi gani mwanangu?”
“Baba ninaomba pesa ya kununua simu kwa ajili ya mawasiliano”
“Sawa”
Baba akatoa kikadi cha banki na akaniandika namba zake za siri kwenye kikaratasi na kumuomba dereva wake anipeleke kwanye ATM za banki na kish yeye akaingia kweye ndani ya gorofa na sisi tukaondoka.

“Kaka hivi simu za gharama huku nitazipata wapi?”
“Maduka yapo mengi tuu utakapo hitaji wewe nitakupeleka”
“Maduka yanatumia pesa aina ya dola au Rand”
“Inategemea na duka lenyewe linatumia pesa ya aiana gani ila ninakushauri ukatoa dola ya marekani”
“Sawa utanirushia zile picha za jana”
“Sawa”

Tukafika kwenye gorofa ambalo lina mashine za kutolea pesa(ATM) na tukashuka ndani ya gari na jamaa akabaki njea na mimi nikaingia ndani.Nikachukua kiasi cha pesa ya kunitosha hata kwa matumizi mengine kisha nikatoka nje na kumkuta jamaa akiminyana na dada aliye na nywele zilizo changuka huku dada huyo akiwa amenipa mgongo na mavazi yake yakiwa yamechafuka na kuchanika chanika sana.Mwili wake umejaa ukurutu na amepauka sana huku ukiwa umedhohofika sana japo anaonekana kuwa na nguvu nyingi na kwaharaka haraka nikatambua kuwa dada huyu ni kichaa.

“Eddy nenda kwenye gari ninakuja sasa hiv....khaaa”
Jamaa alipiga kelele baada ya dada huyo kumng’ata kwanye mkono kisha akanigeukia na mimi na kujikuta nikibaki nikiwa nimesimama huku nikiwa nimemshangaa kichaa huyu kwani ni Sheila mpenzi wangu ambaye mara ya mwisho kumuona ni siku niliyo gongwa na gari.Nikiwa nimesimama Sheila akamuachia jamaa na kunirukia mimi na sote tukaanaguka chini huku nikijitahidi kumshika kichwa chake anacho taka kuning’ata kwa meno yake yaliyo machafu huku akidondosha udenda mwingi na akinguruma kama mbwa mkali mwenye njaa kali....
                               
                      ******SORY MADAM******(34)


Mlinzi akamuwahi Sheila na kumnyanyua juaa na lipindi tukio linatokea askari waliweza kuliona na wakamkamata Sheila na kabla hawajaondoka naye nikawazuia
“Jamani samahani kaka zangu ninamuhitaji huyo binti”
“Huyu ni mwenda wazimu na ametoroka katika hospitali ya vichaa na karibia wiki sasa tunamtafuta”
“Sawa nimewaelewa sijui tunaweza tukaongozana hadi sehemu ilipo hiyo hospitali?”
“Kwani wewe unamfahamu huyu binti?”

“Hapana ila ninahitaji kuweza kuyafahamu maendeleo yake”
Askari wakanitazama kisha wakaniruhusu kama kuongozana nao,tukaingia kwenye gari letu na kuongozana na askari hadi kwenye hospitali ambayo ni yawatu walio pungukiwa na akili.Sheila akakabidhiwa kwa madaktari na polisi wakanionyesha sehemu ambayo ninaweza kupata kawimu za maendeleo ya Sheila,

“Samahani dada yangu”
Nilimuuliza nesi mmoja niliye mkuta kwenye dirisha la kuudumia wateka wanao hitaji huduma kwenye hospitali hii
“Bila samahani”

“Kuna mgonjwa ameletwa dakika tano zilizo pita na ninaomba kuweza kujua takwimu zake za nyuma”
“Ahaaa juyo dada aliyeletwa hapa akiwa hajitambui na kadris siku zilivyo zidi kwenda alikuwa msumbufu anapiga wezake hadi kunasiku alimuua mwenzake mmoja kwa kumpiga kwa chupa kichwani”

Nikajikuta nikiwa nimeuacha mdomo wangu wazi kwa mshangao kwa maana sikutegemea kusikia taarifa kama hiyo
“Labda tatizo leke kubwa haswa ni nin?”
“Mmmm kwa mimi siwezi kujibu labda ngoja nikukutanishe na daktari ambaye alikuwa akimuhudumia tangu siku ya kwanza alipo kuja”

Akanyanyua mkonga wake wa simu na kuzungumza na mtu aliyo upande wa pili wa simu kisha akaniomba niweze kuingia ndani kwenye ofisi ambayo ipo upande wangu wa kushoto na ikanilazimu kumuacha nje dereva,Nikamkuta daktari wa kiume mwenye umri mkubwa kiasi na akaniruhusu nikae pembeni kwenye kiti.

“Nikusaidie nini kijana?”
“Kuna mgonjwa ambaye ameletwa muda mchache ulio pita na sijui ninaweza kupata taarifa yake ya nyuma?”
“Wagonjwa walio letwa muda mcha ulio pita ni wengi labda wewe unamzungumzia yupi kati ya hawa?”
Daktari akawasha Tv yake kwa kutumi rimoti na nikaziona picha za Sheila akiwa ameshikwa na askari
“Huyo picha namba tano”
Nilimuonyesha daktari kwa kutumi kidole na akaizima Tv yake na kunigeukia huku akisaidiwa na kiti chake chenye uwezo wa kuzunguka

“Huyo hapa sisi tunamuita Vaiper Lady”
“Kwa nini?”
“Kwanza nimkali na ninamfananisha na hao nyoka ambao wanasifa ya kung’ata sana,Pili hatulitambui jina lake halisi ni nani”
“Sawa ila tatizo lake ni nini?”
“Huyu binti amedhirika sana kiakili hii ni kutokana na mambo magumu ambayo ameweza kupitia huku nyuma.Pia ubongo wake umetingishika kiasi kwamba imemfanya akili zake kufyatuka”

“Akili yake imetingishika?”
“Ndio ina maana aliweza kupigwa kwa kitu kizito kichwani ambacho kiliipelekea akili yake kucheza kidogo na jambo kubwa la kumshukuru Mungu ni kwamba mishipa ya damu haikuweza kupasuka kichwani mwake”

“Anaweza akapona?”
“Mmmm sidhani kwa maana sisi tumejaribu kutumia ujuzi wetu mwingi ila tumeshindwa ila kitu kibaya zaidi huwa hapendi kuona jinsia ya kiume na alashawahi kufanya tukio la mauaji kwa….”

“Hili nilisha ambiwa……Sasa dokta imi ninahitaji kukaa naye kwa ukaribu sana ili niweze kumtuliza”
“Wewe kijana unahitaji kufa au…..kwa maana hataki kuona jinsia yoyote ya kiume”
“Mimi nitaweza dokta na Mungu akibariki kesho nitakuja kwa kazi hiyo”
“Mmmm kwa kweli si……”
Nikachomo noti mbili za dola mimi kwenye mfuko wa suruali na kumuwekea daktari mezani na akanyamaza
“Kaka utahitaji kiwango kingine zaidi ya hicho nitakupatia”

Daktaria akanyamaza kimya na kushindwa kuzungumza kwa aibu na nikanyanyuka na kumuacha akiwa ananishangaa.Hali ya furaha ikanitoweka kabisa na hata ndani ya gari nikawa kimya huku nikimuwazia Sheila na sikusema kuwa ninamfahamu Sheila hii ni kuepuka maswali mengi yasiyo na msingi kwangu.Tukaingia kwenye moja ya duka la simu na kununua simu aina ya Blackbery.Tukarudi kwenye jengo ambalo baba aliingia na kumkuta akiwa anatusubiri.

“Mbona mumechelewa?”
“Ahaa kuna sehemu sehemu nilipitia”
“Hiyo simu umesha nunua?”
“Ndio baba”
“Sasa turudi nyumbai kwa maana lile swala nimesha likabidhi kwa wahusikana wameniahidi ndani ya siku mbili watanipa jibu”

“Kweli baba?”
“Ndio wewe kuwa na amani na kama utataka kuendelea kutazama tazama mji nipige simu nyumbani nije kuchukuliwa na gari nyingine?”
“Hapana kwanza nimechoka ninahitaji kupumzika kidogo alafu ninaomba namba yako baba”
“Sawa”

Baba akanipatia namba yake ya simu na kutokana sikuwa na line ikamlazimu kunipa laini yake moja ya simu ambayo haitumii sana.Tukarudi nyumbai huku msongamano wa mawazo ukiwa umenitawala na moja kwa moja nikagundua baba wa zamani mzee Godwin ndio chanzo cha Sheila kuwa katika hali kama hii.Sikuweza kupata suingiza kabina na kila nilipo jaribu kuivuta amani kutawala usoni mwangu nikajikutani kishindwa kabisa na sura yangu ikawa imetawaliwa na mikunjo ya hasira.

Nikiwa nemekaa kwenye moja ya masofa ya kupumzikia yaliyopo kwenye bustani yenye maua mengo mazuri na kuna kijibwawa kidogo chenye maji masafi na upepo mwingi nikamuoana mke wa baba akiwa na yule jamaa wa jana usiku wakiwa kwenye moja ya kijijumba kilicho kwa vioo na ndani yake kukiwa na maua mengi yanayo uteshwa kwa masaada wa mwanga wa jua.

Wakanza kushikana shikana na mwisho wa siku wakanza kupeana mambo ya chumbani bila kujali kama wanaweza wakaonekana na mtu.Nilicho kifanya ni kurekodi tukio zima mwanzo hadi mwisho hadi wanamaliza na jamaa akawa wa kwanza kutoka na baada ya dakika kama kumi mke wa baba naye akatoka huku akijifanya kunusa nusa kipande cha ua alicho toka nacho na kwabahati mbaya macho yetu yakakutana na akanipandisha na kunishu kiasi kwamba akaanza kunikera

“Mama ninakuomba”
Akatembea kwa mwendo wa madaha huku mdomo wake akiwa ameubenua kiasi kwamba nikaanza kujiuliza sijui kipigo cha jana amekisaha
“Unasemaje?”
“Hivi baba yangu ni nani kwako?”
“Khaa wewe unamuona ni nani?”

“Jibu nililo kuuliza”
“Ni mume wangu”
“Una uhakika na unacho kizungumza?”
“Ndio kwa maana hata pete hii hapa ninayo”
“Unajua siku zote kwenye maisha usipende kumfanyia mwenzako kile usicho penda kufanyiwa”
“Una maana gani?”
“Utaijua wewe nenda zako”

Akaniandisha kuanzi chini hadi kitendo ambacho maishani mwangu sipendi mwanamke anifanyie akaachia msunyo mkali uliao nifanya ninyanyuke kwa haraka na kumfwata kwa hasira na akaanza kukimbia ila kutonaka na uwezo wangu wa kukimbia nikamdaka katika mlango wa kuingilia sebleni na kukutana na baba akiwa anatoka ndani.

“Huyu mwanao ni mwenda wazimu nini?’
Sikumjibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kumfwata na nilipo sikia swala la uwenda wazimu na mimi nikajichetua sana na ili nionekane ni mwenda wazimu kweli.Tukaanza kazi ya kukimbizana huku tukimzunguka baba aliye kosa kitu cha kuzungumza,
“Mume wangu mkamate mwanao atanijeruhi”

Na mimi nikaanza kuuigilizia mlio wa Sheila alio kuwa akiningurumia na kumfanua baba kuhamako na kadri muda unavyo kwenda ndivyo nikazidi kujichetua kaisi kwamba baba akaagiza walinzi wake kunikamata na wakashauriana wanipeleke hospitali ya vichaa kwa ajili ya vipimo zaidia.Kwa bahati nzuri tukafika kwenye hospitali tuliyo toka masaa machache yaliyo pita na kwabahati nzuri daktari aliye pewa jukumu la kunipima na yule niliye mpa dola mia mbili na akawa ananishangaa kuniona nikiwa nimeletwa kama mgonjwa.

“Dokta wakikuuliza waambie kuwa itanibidi hapa nikae kwa wiki mbili”
Nilimuambia daktari baada ya baba na watu wake kutoka nje ya chumba nilicho ingizwa
“Saaa….saaa”
“Dokta acha kupata kigugumizi wewe waambie hivyo kuwa mimi ni mgojwa na mutaniweka hapa kwa wiki mbili ili kunichunguza zaidi na kama ni pesa mimi nitakulipa ila hili ni dili kati yangu mimi na wewe”
“Sawa nimekuelewa”

Daktari akanipima pima kiuongo ili kupoteza muda kisha akatoka na baada ya muda baba akaingia huku akiwa na sura ya unyongee na kwambali machozi yanamlenga lenga
“Ohhooo Eeeehee baba ukuwaa mkubwaa kamaaaaa John Cennaaaaaa hahaaa…babaaa huuuyoooo katokaaaa kaziiiniiiiiiiii ohooaaooa”
Niliimba nyimbo za kuwehuka na kuzidi kumfanya baba aamini kuwa mimi nimepata kichaa

“Dokta kweli mwangu atapona?”
“Kama nilivyo kuambia hapo awali tunamuweka hapa ndani ya wiki mbili kisha tutaangalia jinsi maendeleo yake yanatavyo endelea”
“Ahahaa doktaaa wiki mbiliiiii hahajhhhaa mimi takaaa kaaaa mwakaa mzimaaaa baaaabaaa lia liaaa kama totojingaaaaaa hahaahaa”

Nikazidi kuzungumza huku nikirusha rusha miguu na mikono na ikawalazimu watu wa baba kunilaza kitandani na kunifunga mikono na miguu kwa kitumia mkanda maalumu uliopo juu ya hichi kitanda nilicho lalia.

“Ohoo Mungu wangu sijui ni kitu gani kimempata mwanangu?”
“Usiwe na wasi wasi atapona tuu cha msingi ni kumuomba Mungu aweze kumjalia afya njema”
Baba akanitazama kwa sura ya simanzi na akashindwa kuyazuia machozi yake na akaanza kulia na ikamlazimu mlizi wake mmoja kutoa kitambaa na kumkabidhi baba kisha akatoka naye nje na walinzi wake wengine wawili wakafwatia nyuma.

“Dokra wachungulie wamesha ondoka?”
“Ngoja niangalie”
Dokta akafungua mlango na kuchungulia kisha akaufunga na kunifwata kitandani huku akiwa anacheka
“Ndio wamesha ondoka….hivi wewe kijana mbona msanii kiasi hichi?”

“Ahaaa uanajua unapo amua kufanya kitu mtu inabidi uweze kufanya juu chini unakifanikisha hata kwa staily kama hii pia ni vyema si umeona sasa mpaka mzee ame….hahaaaa chipissssisisisisiiii oohoooo”

Nilirudi katika hali yangu ya kuchanganyikiwa baada ya mlango kufungulia na wakaingia majamaa wawili wenye misuli na wamevalia makoti meupe na suruali nyeupe
“Huyo naye dokta ana tatizo gani?”
“Ahaa mchukueni mumpeleke kwenye chumba chake”

Jamaa wakanifungua mikanda na kuninyanyua kwa nguvu na mmoja akanishika mkono wa kulia na mwengine mkono wa kustoto,tukatoka nje ya chumba na kuwaona baba na watu wake wakija kwenye ofisi ya daktari na ikanilazimu nianze kuchetuka kama kawaida huku nikijirusha rusha juu na kuwafanya majama hawa kutumia nguvu zaidi katika kunibana,Baba akawaomba wasimama kisha akasimama mbele yangu na kunitazama kwa muda huku akijikaza kuto kulia.Akanikumbatia na kuwaruhusu jamaa wanipekeleke wanapo nipeleka.

Nikaanza kupata woga kwa maana kila nilipo pita vichaa wakiume walianza kushangilia huku wengine wakiwa na sura za ajabu ajabu
“Sasa dokta naye tulimuuliza anatatizo gani huyu hajatujibu sasa tutampeleka kwenye wodi gani?”
“Kwa jinsi ninavyomuona tumuingize wodi namba nano itamfaa”

Jamaa wakashauriana na kweli wakaniingiaza kwenye wodi yenye vitanda vingi na vingi vinawatu ambao kwa muonekano wao ni vichaa walio pitiliza na mbaya zaidi wengi wana miili mikubwa kupita maelezo kiasi kwamba kila nilipo pita walinitazama kwa macho makali.Jamaa wakanionyesha kitanda changu kisha wakatoka kwa haraka huku wakionekana kujishuku.Majamaa matatu yakasimama kwenye vitanda vyoa na kuanza kupiga hatua za kunifwata kitandani huku ikinguruma kama mimbwa inayo gombania mke mmoja,mapigo ya moyo yakazidi kunidunda huku kijsho kikinimwagika kiasi kwamba ubabe wangu wote ukaniishia.

Majaa yakanitazama kwa muda huku yakinguruma na yakaanza kunishika shika kichwa changu huku kila mmoja akitaka nimtazama yeye,Nikastukia kofi moja takatifu likitua kwenye sikio langu na kusababisha uwezo wa kuona vizuri ukakata na kuona vitu vyenye alama kama nyota nyota vikielea angani kiasi kwamba nikajikuta nikiona giza lililo endana na ukungu.

Nikastukia nikiwa nimelala chini sakafuni wala sikujua nimeshuswaje kwenye kitanda.Makelele ya vichaa wengine yakazidi kunichanganya kiasi kwamba nikawa sielewi nini cha kufanya.Kipigo kutoka kwa haya majamaa ambayo yanaonekana ni mababe kwenye hii wodi kikanifanya nijikunyate huku nikilia kwa uchungu.Nikaingia chini ya uvungu wa kitanda ili kujinusuru kwani inadi ya vichaa wanao nishambulia ikaongezeka,Nikastukia nikivutwa miguu yangu na wakaanza kuniburuza huku wakishangilia kwa nguvu.

Maumivu makali yakazidi kuniumiza kiasi kwamba nikajuta kwa uamuzi nilio uchukua.Wakanigongesha gongesha kwenye kwenye vitanda kisha wakanilaza kwenye kordo iliyo tenganishwa na vitanda na wakanizunguka huku wakinitaza na vijamaa viwili vyembaba vikapanda juu ya vitanda nawezao wakaacha nafasi na sikujua wanataka kufanya nini,Nikastukia wa kwanza akijirusha na kunifanya nimkwepe na akapiga kichwa kwenye sakafu na kutulia tuli.Wa pili akafanya kama alivyo fanya mwenzake na akanitulia kwenye tumbo na kunifanya nitoe ukulele mkali wa maumivu huku kicha kizima kikiwa kimejaa manundu ya kipigo nilicho kipata.

Nikastukia wakianza kunikojolea huku wakicheka kwa furaha na kupeana mikono na kunifanya nizidi kulia kwa uchungu japo hasira imenipanda sikuwa na uwezo wa kufanya chochote dhidi yao.Wakatawanyika na kuondoka kila mmoja akarudi kawnye kitanda chake na wakaniacha nikiwa nimejilaza chini pamoja na kale kajamaa lalicho nirukia.Nikaanza kujivuta taratibu hadi kwenye kitanda changu huku mwili mzima ukiwa ninanuka mikojo pamoja na kuvimba juu na nikakaa na baada ya muda mlango ukafunguliwa na wakaanza kutoka mmoja baada ya mwengine.Akachugulia daktari mmoja na kutuona ndani ya chumba tumebaki wawili na baada ya muda wakaingia madaktari wanne ambao wawili wakanifwata mimi na wawili wakaenda kwa kale kalicho zimia.

“Huyu ni mgeni eheee?”
“Naona”
“Ahaaa wageni huwa wanapata shida sana”
“Kweli kwa maana walivyo mfanya mmmm ni zaidi ya maumivu”
Madtari wakaendelea kuzungumza huku wakinihudumia na kuniweka kwenye machela na kunihamisha kwenye na kuniingia kwenye chumba cha matibabu.

Ndani ya siku nne nikawa nimepona vuzuri japo sio sana kwani kuna baadhi ya sehemu zinamaumivu kidogo.Nikarudishwa kwenye wodi ambayo nilitembezewa kichapo na nikaanza kazi yangu rasmi ya kumtafuta Sheila kwenye kila sehemu ya hospitali hii,Ndani ya siku mbili sikuweza kumuona Sheila na sikujua ni wapi alipo,Nikaanza kuzoeana na vichaa kadhaa ambao ni wanyonge kama mimi kwa maana jinsi watu wanavyo ishi kibabe kwenye hii hopitali inasababisha kuwemo na mgawanyiko wa vichaa wababe na vichaa wanyonge.Wakati wa kuoga ukawadia na kama kawaidi kila wodi ina mabafu yake ambayo muda wa kuoga unapo wadia ni wote tunatakiwa kufanya hivyo.

Nikatafuta sehemu isiyo na mminyano na kusimama na kuwatazama jinsi vichaa wengine wanavyo minyana kwenye kuoga.Wakaoga wote kisha wakatoka na mimi nikanza kuvua nguo zangu na kabla sijamaliza kuzivua akaingia lile jijamaa ambalo lilinizaba makofi pamoja na wezake na baada ya kuniona likaanza kunguruma na kuanza kunifwata na nikajiandaa kwa chochote atakacho hitaji kukifanya kwangu mimi.Likanisimamia mbele yangu huku likinitazama kisha likanitisha kama ninataka kunipiga kofi na kujikuta nikiinama huku mikono yangu nikiwa nimeiweka kichwani kuziba uso wangu na nikastukia likaanza kucheka sana hadi likakaa chini kwa kucheka na ikanibidi na mimi kuanza kucheka

Hata hamu ya kuoga ikaondoka na kujikuta nikivaa nguo zangu na kutoka bafuni.Kama kawaida muda wa michezo ukawadia na kila kichaa anaye penda mchezo wake anakwenda kwenye eneo lenye kiwanja cha mchezo wake.Nikaanza kuzunguka zunguka nikaangalia jinsi vichaa wanavyo fanya mambo ya ajabu kusema kweli inahitaji moyo wa uvumilivu kuishi nao kwa maana kama akili yako ni nzima basi ukishindwa kuvumilia unaweza ukawaambia madaktari kuwa umepona.Nikakuta wasichana watatu vichaa wakiwa wamekaa chini wakichora chora na katika kuwachunguza vizuri nikamuona Sheila akiwa katikati yao

Na mimi nikajisogeza karibu yao na kukaa huku nikimtazama Sgeila jinsi anavyo chora chora cini kwa kkutumia kijiti huku akifuta futa.Wezake wakasimama na kuondoka zao na akabaki peke yake.Sheila hakuinyanyua sura yake kunitazama na akazidi kuchora chini huku akikigandamiza sana kijiti chini na akiwa anaonekana kama anahasira kali.Machozi yakaanza kumwagika kiasi kwamba akafuta alicho kichora kicha akaanza kuandika herufi moja moja kwa uchungu{I…….L…..O…….V…….E}

Nikabaki nikimuangalia huku kwa mbali na mimi machozi yakinilenga lenga kwani afya yake imedhohifika sana isitoshe mwili wake umetawaliwa na makovu mengi sana ambayo yamemfanya azidi kuonekana mbaya.Akayafuta maandishi yake kisha akachora vikatuni viwili kimoja kikiwa cha kike huku kingine kikiwa cha kiume na akavipatia majina kwa herufi za mwazo ambacho kikatuni cha kike akakiandikia herufi kubwa ya ‘E’ huku cha kike akikiandikia kiherufi cha ‘S’.Hapo ndio nikashindwa kuzizuia hisia zangu na kujikuta nikimwagikwa na machozi na kumuona Sheila akiinyanyua sura yake tartibu na kuniangalia kwa muda kisha akairudisha sura yake chini na akanitazama tena kwa umakini huku akiwa kama mtu anaye jitahidi kuvuta kumbukumbu ya kitu fulani ila anashindwa kujua ni nini anacho kiwazia

“Sheila…..Sheila?”
Akaonekana kustustuka na akanikazima macho hadi akaanza kuniogopesha akajaribu kuzungumza ila akawa kama anashindwa.Aafuta vidoli vyake chini na kuandika maandishi yaliyo nistua zaidi.

{MIMI SIWEZI KUZUNGUMZA NIPO SAWA SAWA NA BUBU}
Maumivu makali yakapenya kwenye moyo wangu na kujikuta sura nzima ikitawaliwa machozi.Nikachukua kijiti chake na kumuandikia chini
{KWANINI HUWEZI KUONGEA?}
Sheila akanitazama kwa macho ya mshangao kwa jinsi ninavyo lia kisha akaniandikia chini
{SIWEZI TUU KWANI NILILISHWA MAKAA YA MAWE KWENYE MDOMO WANGU}

Sheila akaufungua mdomo wake na kuutoa ulimi wake nje na nikajikuta nikitetemekwa kwa woga kwani ulimi wake una majeraha makubwa yanayo onyesha vika ni kweli alilishwa makaa ya moto.Sheila akasimama gafla na ni mimi nikasimama na akaanza kutembea na kujikuta nikizidi kuumia kwani hata shepu lake la nyuma lilidhohofika sana.Tukaongozana hadi kwenye moja ukumbi ambao kuna kiwanja cha mpira wa kikapu(basketball) na akazidi kunipeleka hadi kwenye moja ya mabafu na akanitazama na kulivua gauni lake

Nikajikuta hata uwezo wa kuhema ukianza kuwa mdogo kutokana na mstuko nilio upata baada ya kuuna mwili wa Sheila ulivyo jaa majeraha makubwa ya kachanwa chwana na kutu chenye ncha kali.Akanigeukia mgongoni na kunionyesha kuvu kubwa la kutobolewa huku ngozi ya sehemu hiyo ikiwa imekunjamana na kujikuta nikizidi kuteswa na uchungu,Macho ya Sheila yakaanza kuvunjwa na machozi na akatazama tazama ndani ya bafu hili na sikujua anatafuta nini.Akafungua koki ya bomba la maji kisha akachovya kidole chake kimoja ndani ya maji na kuandika kwenye kiio kikubwa kilichopo ukutani.

{MIMI SIO KICHAA ILA WATU WANANIISI KUWA MIMI NI KICHAA ILA UKWELI NI KWAMBA NINAAKILI ZANGU VIZURI NA HAYA YOTE YAMETOKANA NA MAUMIVU MAKALI NILIYO PEWA NA MZEE MMOJA AMBAYE NI MKUU WA JESHI NA NIBABA WA MPENZI WANGU EDDY}
Sheila akanigeukia na kuniuliza kwa ishara kama nimeelewa alicho kiandika na mimi nikatingisha kichwa nikimuashiria kuwa nimeelewa

“Unanikumbuka?”
Nilimuuliza Sheila na akabaki akinitazama kwa muda kisha akachovya kidole chake kwenye maji na kuandika kwenye kioo
{HAPANA ILA NINAKUFANANISHA NA EDDY WANGU ILA SIO WEWE KWANI YEYE ANAAKILI ZAKE TIMAMU NA SIO CHIZI KAMA ULIVYO WEWE}

Nikatulia kwa muda huku nikiyatafakari maneno ya Sheila aliyo toka kuniandikia muda mchache ulio pita.Nikamsogelea Sheila na kumkumbatia huku nikiwa ninamwagikwa na machozi.Mlango ukafunguliwa na wakaingia madaktari wawili wa kiume na walivyo tuona tumekumatiana wakanitoa mimi kwa nguvu na kuchomoa virungu vyao na kuanza kunipiga huku wakiniburuza na kunitoa nje
“Sheila….nisaidie ninakufa mimi”

Nilizungumza kwa sauti ya juu huku nikiwa ninalia kwa uchungu na kuzidi kuwaongezea hasira madaktari hawa na kuzidi kunipiga,Sheila kwa haraka akatoka huku akiwa na nguo ya ndani na akamsukuma dokta mmoja ana akajibamiza kichwa ukutani na akaanguka chini kisha akamshika kichwa cha gaktari na kunaza kukibamiza kwenye sakafu kwa nguvu hadi kipasukwa kwenye kisogo chake,Daktari aliye kuwa anaendelea kunipiga baada ya kumuona mwenzake akiwa anaaga dunia akaniacha na kwa nguvu zake zote akarusha kirungu chake na kikatua kichwani mwa Sheila na akadondoka chini na damu za puani zikaanza kumwagika


ITAENDELEA...

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!