Tuesday, August 2, 2016

Shetta Ajihadhari kutoa Ngoma mbaya kutokana na Ushindani Mkali katika Muziki

Hit maker wa wimbo ‘Namjua’ Shetta amefunguka kwa kusema kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao hawajawai kutoa ngoma mbaya katika maisha yake ya muziki.
 
Akiongea nasi Jumapili hii, Shetta amesema biashara ya muziki imefanya afanye muziki wa kushindana kila siku ndio maana kila akitoa ngoma anahakikisha ni kali.

“Shetta sasa hivi ni mfanyabiashara, muziki wangu ni bidhaa adimu ndio maana mimi sijawahi kutoa ngoma alafu isifanye vizuri, ni hit baada ya hit na ndo maisha yangu kwa sasa, na nitaendelea kufanya hivyo,” alisema Shetta.

Rapper huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kubiria surprise ya wimbo wake mpya baada ya ‘Namjua’ kufanya viruri.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!