Thursday, August 11, 2016

Snura Akiri Kusumbuliwa Sana na Wanaume wanaotamani Mauno yake

Msanii Snura ambaye mara nyingi amekuwa akikumbwa na rungu la BASATA kutokana na video zake ambazo zinakuwa na utata, amesema mauno ambayo BASATA 'wanamind' ndio yamemfikisha hapo alipo.
 Snura amesema mauno yake ndiyo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuinua muziki wake, kutokana na jinsi anavyoyamwaga akiwa jukwaani, na kuwavutia mashabiki wake.

"Nimeimba sana lakini kiuno changu kimenisaidia sana kunitambulisha, ukisikia kuna show ya Snura jua mauno yanamwagwa kweli, na sijaanza leo nilianzia kwenye ngoma za asili", alisema Snura.

Snura aliendelea kusema kuwa ingawa mauno hayo humpa wakati mgumu akiwa kwenye kazi zake kutokana na uchu wa baadhi ya wanaume wanaomsumbua, lakini amekuwa akijitahidi sana kujilinda ili asiharibu kazi yake.
 
"Usumbufu kiukweli upo,wengine wananipenda kweli wengine wananitamani, kikubwa nazingatia sana kazi yangu, nashinda sana vishawishi kwa sababu vile ninavyokatika wengine wanadhani nafanya promotion ya biashara", alisema Snura.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!