Saturday, August 13, 2016

Vera Sidika Atoa Angalizo Kwa Wasichana Kuhusu Matiti na Makalio Feki

Mlimbwende ambaye anasumbua katika mitandao ya kijamii kutokana na shepu yake ya kibantu pamoja na kuweka matiti feki, Vera Sidika amewakanya mabinti wengine kutofuata yale aliyoyafanya, kwani wanaweza wakajiingiza kwenye matatizo.

Akizungumza kwenye FNl ya East Africa Television, Vera Sidika amesema yeye aliamua kujiongeza matiti yake ili awe na mwili unaoendana na jinsi alivyo kwenye hipsi zake, lakini wengine wasithubutu kufanya hivyo kwani wanaweza kupata maradhi kama saratani.

“Wasichana wasijaribu nilichokifanya, kwa sababu si kila nilichofanya mimi unaweza kufanikiwa, mimi niliweza kuaford na kwenda kwa wataalam, kwa watu wengi ambao hawawezi kuaford bei ya sugery wanaweza wakaenda kwa watu wasio na utaalam, kisha wakapata madhara”, alisema Vera Sidika.

Vera amesema aliamua kufanya ‘plastic surgery’ ya matiti yake kwani alikuwa na kifua kidogo, hivyo alitaka awe na kifua ambacho kinaendana na shepu yake ya chini, na ilimgarimu dola elfu 30 kufanya hivyo nchini Marekani.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!