Monday, September 26, 2016

Lipumba kushtakiwa Baraza Kuu la CUF

Kamati ya Utendaji ya Taifa ya Chama cha Wananchi (CUF), imeandaa ajenda ya kumfikisha Prof. Ibrahim Lipumba mbele ya baraza kuu la uongozi wa chama hicho ili ajieleze kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvunja na kuvamia ofisi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Nassor Ahmed Mazrui imesema kutokana na kitendo cha kuvamia ofisi kuu ya chama hicho Jijini Dar es Salaam, kusababisha uharibifu wa mali hivyo kesho kamati hii itakaa kwa ajili ya kujua mustakabali wa chama hicho.

Mazrui amesema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ya mwaka 1992 kamati ya utendaji ya taifa imeandaa ajenda na kumfikisha Prof. Lipumba mbele ya baraza hilo ili ajieleze kwa nini asichukuliwe hatu za kinidhamu kwa mambo aliyoyafanya.

Katika hatua nyingine Mazrui amesema kamati hiyo imekataa maoni na ushauri uliotolewa na msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mtungi ambaye amesema kuwa ofisi hiyo inamtambua Prof. Lipumba kama mwenyekiti halali wa chama hicho.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!