Wednesday, September 21, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 53 & 54 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa


Ilioishia....
Nikanyanyuka na  kukifunga kibegi changu, nikatizama kwenye kioo cha computer yake, iliyopo juu ya meza yake, kilicho gawanyika katika vipande sita vya picha za video za kamera za ulinzi na kuona gari aina ya rangerover ikisimama kwa kasi  nje ya benki na wakashuka wasichana watano walio valia mavazi meusi huku wakiwa na bunduki mikonini mwao.Wakanza kuwashambulia askari huku walili wakiingia ndani ya benki na kuanza kuwashambulia askari na kuwaamrisha watu wote kulala chini.Nikamuona wakimuamrisha bwana turma kuingia kwenye chumba ambacho ndicho wanahifadhia pesa.

Endelea....
Japo ninaroho kidogo ya kikatili, ila kwa jinsi risasi zinavyo ngurumishwa nje na majambazi hawa, sikuthubutu hata kujaribu kutoka ndani ya chumba.Bastola yangu nikaishika vizuri kwa umakini huku macho yangu yakitazama kwenye kioo cha computer iliyopo juu ya meza.Nikawashuhudia wasichana wawili wakimuamrisha bwana turma kuingia ndani ya chumba ambacho ni chakuhifadhia pesa.Wakaendela kuingiza pesa kwenye mifuko yao, nikamuona msichana mwengine akiingia akiwa na bunduki.Sikusikia kitu anacho kizungumza.Nikaanza kusangaa baada yakuwaona watu wakivuliwa nguo na kupangwa mstari katika mlango wa kutokea nje
“wanataka kufanya nini hawa?”

Nilijiuliza swali ambalo jibu lake nikalipata  baada ya kuona watu wakitolewa nje wakiwa uchi pasipo kuwa na nguo hata moja kwenye miili yao.Wasichana wakajichanganya kwenye kundi kubwa la watu wanaotoka wakiwa, wanakimbia.Nikaitumia nafasi hiyo na mimi kutoka ndani ya chumba huku kibeki changu nikiwa nimekifunga vizuri na kukishika kwenye mkono wangu wa kushoto huku mkono wangu wa kulia nikiwa nimeishika bastola yangu.Nikajichanganya kwenye watu na kukimbilia lilipo gari letu,nikamkuta dorecy akiwa amejiinamia kwenye gari, nikafungua mlango wa gari na kuingia ndani

“eddy vipi huko?”
“tuondoke, sikwema huku”
Nikawasha gari na kuliingiza barabarani kwa kasi ya hali ya juu,
“eddy tunaelekea wapi?”
Dorecy aliniuliza huku akinitazama kwa macho makali, sikulijibu swali lake zaidi ya kuongeza mwendo kasi wa gari langu.Nikafika maeneo ya mataa na kukuta msongamano wa magari mengi yakiwa katika foleni
“shiitii”

Nilizungumza huku nikiitizama gari ndogo ya polisi inayokuja nyuma yangu kwa kasi, wakionekana kunifwatilia mimi.Kutokana nyuma yangu hakuna gari, nikairudisha nyuma gari yangu, na kuingia barabara ya pili inayopitwa na watembea kwa miguu, kazi yangu ikawa ni kupiga honi, huku nikiwa makini katika uendeshaji wangu.Watu wengi wakawa na kazi ya kulikwepa gari langu huku wengine wakijirusha kwenye mitaro kuepuka kifo
“eddy angalia mbelee”

Dorecy alizungumza kwa sauti kubwa, kwani kuku gari la abiria linakuja mbele yetu kwa mwendo wa kasi, kwa haraka sana nikakunja kushoto na kuzibaniza pikipiki za waendesha bodaboda zililozo pangwa barabarani wakisubiria wateja, kwa kupitia kioo cha pembeni, nikalishuhudia gari la abiria lilipoteza muelekeo na kuyakuma magari mengine na kusababisha ajali mbaya.Kwa ukubwa wa gari yangu haikuwa shida sana kuzikanyaga pikipiki mbili zilizopo mbele yangu.

Nikapata kiupenyo cha kuingia barabarani na cakumshukuru mungu, hakuna magari ya foleni ambayo yanaweza kunizuia kuendelea na safari yangu, huku nikiwaacha waendesha pikipiki wakitoa matusi mengi juu yangu
Kwa mbali nikaliona gari, walilokuja nalo majambazi likichanja mbuga barabara ya kuelekea mkoani

“wale ndio majambazi walio piga tukio benki”
Nilizungumza huku nililiinyooshea kidole gari la majambazi aina ya rangerover.
“mmmmm”
Dorecy aliguna, huku akinitazama machoni.Nikazidi kukanyaga mafuta na kuzidi kulisogelea majambazi, ambalo nalo linakwenda kwa mwendo wa kasi sana.

“eddy kuwa makini, wasije wakatushambulia”
“powa”
Sikuona gari yoyote ya polisi inayokuja nyuma yetu, nikazidi kulifukuzia gari la majambazi na gafla likakunja na kuingia porini
“eddy nyoosha tuu, tusiwafate”
“powa”
Nikaachana na gari la majambazi na kuelekea zangu barabara inayokwenda mikoa ya tanga na arusha.Kwa mbali nikawaona askari usalama barabarani wakiwa wamesimama.

“eddy punguza mwendo”
“huoni kama tutakamatwa?”
“nitazungumza nao mimi”
“dorecy”
“fanya hivyo, la sivyo itakuwa ni tatizo kubwa”
“powa”

Nikapunguza mwendo wa gari, na askari mmoja akatusimamisha, nikalisimamisha gari langu pembeni na askari huyo akaanza kuja kwa mwendo wa umakini, huku akilitazama gari langu.Nikaishika bastola yangu kwa umakini, ila dorecy akaushika mkono wangu wa kushoto ulio shika bastola

“tulia”
Dorecy alinizuia kufanya ambacho ninahaji kukifanya, kwa ishara askari akaniomba nifungua kioo cha gari upande nilio kaa mimi, nikatii kama alivyo hitaji mimi kufanya
“habari yako afande”
Jamaa alianza kunisalimia, nikaachia tabasamu pana ambalo muda wowote ninaweza kulibadilisha
“salama tuu, kaka”

“mbona gari yako, mbele kidogo imebonyea?”
“ahaaa kuna, mjinga alinibamiza kwenye mataa kule”
“ahaaa, munaelekea wapi?”
“nakwenda, tanga mara moja kuna kazi hapo tumeagizwa na rpc”
“kuna, gari tunaiwinda ya majambazi wamepiga tulio benki, ndio tupo tupo hapa, tunaisubiria”
“ipoje hiyo gari?”
Polisi akaniwasha simu yake na kunionyesha picha cha gari hilo

“nimetumiwa whatsap hii picha”
Dorecy akaitazama picha ya gari ambalo, tulikuwa tumeongozana nalo
“hii gari tumeongozana nayo”
Dorecy aliropoka na kunifanya nimgeukie na kumtazama kwa macho makali yaliyo jaa mshangao ndani yake
“imengia wapi?”
Dorecy akaanza kumuelekeza askari gari sehemu ilipo ingia, askari akawajulisha wezake na sisi tukaondoka.

“dorecy umefanya nini?”
“kwani tatizo lipo wapi?”
“sio tatizo lipo wapi, wewe inakuwaje unawachomesha watu wa watu katika ishu zao”
“sio ishu zao, kumbuka hata mimi ni askari”
“hata kama”
“sio hata kama, wewe hukuona ni watu wangapi walio uliwa nje ya benki”

“ila sijapenda hiyo tabia sawa”
“eddy, kumbuka hata wewe ni muhalifu”
“so”(sasa)
Nilimjibu dorecy kwa kifupi, huku nikiwa nimekasirika sana
“sihitaji hicho kibesi chako”
“unasemaje wewe?”
“sihitaji hicho kibesi chako cha kijinga, nitakubadilikia sasa hivi, umenielewa?”

Dorecy alizungumza kwa sauti ya ukali, huku akinitazama kwa hasira.Kwa kona ya jicho la kushoto nikamtazama dorecy na kugundua hajafunga mkanda, nikaongeza mwendo wa gari, gafla nikafunga breki za kustukisha na kumfanya dorecy kupiga kichwa kwenye dasbord ya gari.Kwa haraka nikamuwahi kumshika shingo yake na kuiminya kwa nguvu

“huwa sipendi, ujinga kwenye yangu maisha sawa?”
Niliminya dorecy shingo yake kwa nguvu, huku nikimtakandamiza kwenye kwenye siti yake.Nikazichomoa bastola zake katika sehemu alipo ziweka, na kuziweka upande wangu.

“wewe ni nani?”
Nilizumuuliza dorecy huku nikiendela kuminya kwa nguvu kwenye siti yake aliyo kalia.Dorecy akawa na kazi ya kuushika mkono wangu ulio ishika shingo yake
“ed...Eddy ni...Aachi...Ee”
“nitakuua, mwehu wewe”
Nikamuachia dorecy, akaanza kukohoa huku akihema kwa kasi kwani kwa jinsi nilivyo mkaba ni nusu ya kuyaona mauti
“upo na mimi, au?”

Nilimuuliza dorecy na kumfanya aendelee kukohoa, nikabaki nikiwa nimemtazama kwa macho makali kama ya simba dume aliye uliwa mke wake, dorecy akanitazama kidogo kisha macho yake akayakwepesha tena na macho yangu na kutazama chini huku akiendelea kukohoa.Nikaichukua bastola yangu na kumuelekezea dorecy ya kichwa huku nikiwa nimeikandamiza kwenye nywele zake, nikamshuhudia dorecy akitingishika mwili mzima

“nimekuuliza, upo na mimi au?”
“nipo na wewe”
Nikaachia msunyo mkali na kuishusha chini bastola yangu na kuwasha gari langu na kuendelea na safari.Hadi ninafika segera ikanilazimu kusimamisha gari kwani sikujua ni wapi nielekee, kwani arusha siwezi kwenda kutokana ninatafutwa.

“mbona umesimamisha gari?”
“nafikiria kwa kwenda”
Sote tukabaki kimya, kwa wakati huu sikuwa na uwe wa kwenda alipo mama, kwani sijajipanga vizuri na ukatili wa mzee godwin ninatambua vizuri sana, na nikienda kichwa kichwa ninaweza kufa nikiwa ninajiona.

Twende tanga”
Dorecy alizungumza
“unapajua?”
“ndio, kuna rafiki yangu kule atanisaidia pia kwa hili swala lako”
“unamuamini?”
“ndio eddy”
“pita basi huku, uendeshe hari kwani mimi sipajui tanga”
“sawa”

Dorecy akashuka kwenye gari na mimi nikahamia kwenye siti yake.Akaingia kwenye gari na safari ikaendelea, ila kwa muda wote nipo makini sana na dorecy kwani anaweza kubasilika wakati wowote ikawa ni tatizo jengine kwangu
“ulishawahi kufika tanga?”
Dorecy alizungumza
“hapana, ndio leo ninakwenda”
“sawa”
“kwa nini, umeniuliza hivyo?”
“hapana, nilihitaji kujua tuu kama ulisha wahi kufika”

Nikamtazama dorecy kwa umakini, kisha nikashusha pumzi nyingi.Safari ikaendelea huku nikimuomba mungu, dorecy asije kuniyumbisha hata kidogo kwenye mpango wangu wa kumuokoa mama yangu, ambaye siamini kabisa kama mzee godwin amemuua hadi sasa hivi.Japo ninausingizi mzoto, ulio tokana na uchovu wa hekaheka za jana hadi sasa hivi, sikuweza kabisa kuyaruhusu macho yangu kufumba kwani, litakuwa ni kosa kubwa sana kwangu na sukujua ni kitu gani ambacho dorecy anakifikiria kichwani kwake kuhusiana na mimi.

Kila ninavyo jizuia kuyafumbua macho yangu, ikafikia kipindi nikajikuta nikishindwa kuvumilia, nikaiminya kidogo siti yangu kwa nyuma na kuiegemea vizuri na kulala, gafla nikamuona mzee godwin akiwa amemshika mama yangu na kumuweka juu ya meza kubwa, akaipanua miguu ya mama juu ya meza huku akisaidiana na watu wake, akaanza kumkita misumari, mirefu ya miguuni kisha, akampigilia misumari mingine kwenye viganja vya mikono yake, pembeni yupo madam mery na manka wakishangilia jinsi mama anavyo fanywa
“muue, kwani hata yeye mwanaye ameniulia mume wangu kikatili sana”

Madam mery alizungumza huku akishangilia na kupiga makofi akifuahia sana kitendo kinacho endelea.Mama akazidi kulia kwa uchungu, huku damu nyingi zikiwa zinamiminika katika miguu ya viganja vya miguu yake
“nimekuambia chinja kabisa huyo”
Madam mery aliendelea kushangilia, madam mery akachukua mashine ya kupasulia miti mikubwa na kumkabidhi mzee godwin
“weka dishi la maji chini”

Mzee godwin alizungumza, manka akalisogeza dishi la maji chini ya meza na kuliweka vizuri, na damu za mama zinazo toka kwenye mikono yake zikaanza kuingia ndani ya dishi.Mzee godwin akaanza kuiwasha mashine ya kukatia miti hadi ikawaka, kwa kutumia mashine ya kukatia miti akaanza kuukata mguu wa kulia wa mama, na kuzidi kukizidisha kilio cha mama.Akaendelea kuikata miguu ya mama miguu ya mama.

Hakuishia hapo, kwa kutumia mkasi mdogo akaichana tisheti ya mama na kumuacha kifua wazi, akalishika zima moja la mama, akalinyonya kidogo kisha akachukua kisu kikali alicho kabithiwa na msaadizi wake na kukilikata zima la mama upande wa kulia jambo lilizidi kumuongezea mama uchungu, akaendelea kulia kwa maumivu anayo yapata.

“g niue tu, kuliko kunitesa hivi”
Mama alizungumza kwa sauti iliyo jaa vilio, mzee godwin na watu wake wakaanza kucheka kwa dharau akiwemo, manka na madam mery.
“unataka kufa?”
“bora nife, kuliko kunifanya hivi”

Mzee godwin akalitupa ziwa la mama alilo likata ndani ya beseni, kisha kwa nguvu akakichoma kisu chake, tumboni mwa mama na kuuanza kumchana hadi utumbo wake ukatoka nje, kwa kutumia mashine ya kukatia miti akakikata kichwa cha mama na kukitenganisha na mwili wake
“nooo”

Nilizungumza kwa nguvu, huku nikistuka na kujikuta nikiwa ndani ya gari, jasho jingi likazidi kunimwagika na kulisababisha shati langu la pilisi kulowa kama nimemwagiwa maji mengi.Nikaendelea kutasikilizia mapigo ya moyo jinsi yanavyo kwenda, huku nikiwa nimetizama chini, nikageuza shingo yangu upande alio kaa dorecy na sikumku.Nikanyua kichwa kwa haraka huku nikiwa na wasi wasi na kukuta gari ikiwa imesimama nje ya kituo cha polisi kilicho andikwa kwa maandishi makubwa
{kituo cha polisi chumbageni tanga}

Nikamuona dorecy akitoka nje ya kituo, akiwa ameongozana na askari watatu wenye bunduki mikononi mwao, huku akinyoosha kidole sehemu ilipo gari, nikajaribu kufungua mlango ila nikashindwa na polisi nao kwa mwendo wa umakini wakazi kuisogelea gari yangu....


                               *****sory madam*****(54)

.....Nikazidi kuchanganyikiwa, kwa jinsi askari wanavyo isogelea gari langu kwa umakini.Nikajipapasa mifukoni mwangu sikukiona bastola zangu jambo lililoufanya mwili wangu kupoteza nguvu zote na kubaki nikiwa ninawatizama hadi wanafika kwenye gari.Dorecy akawa wa kwanza kufungua gari na kuingia huku akishusha pumzi.

“jamani, huyu ni shemeji yenu, anaitwa eddy, eddy hawa ni rafiki zangu nilikuwa depo so ndio nimepitia hapa kuwaona”
Nguvu zote za mwili zikazidi kudidimia kwani nilidhani kuwa jamaa wamekuja kunikamata kwa makosa niliyo yafanya
“kaka habari yako?”
Askari mmoja alinisalimia, hata nguvu za kumuitikia sikuwa nazo zaidi ya kukitingisha kiwachwa changu nikimaanisha kwamba nimemuitikia salamu yake

“unaonekana umechoka mume wangu?”
Dorecy alizungumza huku akinishika kidevu changu
“yeaah”
Nilijibu kwa upole mwingi
“kaka, mtunze bwana dada yetu, wewe si unaona jinsi alivyo mchuma wa huakika”
Askari mmoja alizungumza huku akiachia tabasamu usoni mwake
“musijali kwa hilo”

Niliwajibu, kidogo hali yangu ikaanza kunirejea, hata mapigo ya moyo kidogo yakabadili muelekeo wake na kurudi katika mapigo yake 72 kwa dakika
“huyu dada yetu kipindi tupo depo, moshi alihamishwa na kupelekwa jwtz”
“kaka, hivi huchezei makofi mawili matatu, kwa maana shosti alikuwa mkorofi huyo”
Sote tukajikuta tulicheka, kwa maana sikutarajia kuwa hawa jamaa muda huu nitakuwa ninacheka nao kwa furaha kiasi hiki.

“hapana jamani, ubabe nimeacha siwezi kumpiga mume wangu, mwenyeni ninampenda kama nini?”
“ahaaa dorecy leo unapenda, kwa maana ninakumbuka afande nyendeza alikutongozaga kipindi tupo porini, acha umporomoshee mangumi”
“hahaaaa, yule alikuwa mwehu, eti ananitongoza huku ananilazimisha kuninyonya denda hapo hapo, kwa nini nisimpige mangumi”

“ahahaa, jamaa tulikuwa naye hapa chumbageni, ila alihamishwa mwaka jana kapelekwa handeni huko”
“dooo, muache akakutane na watoto wa kizigua wamroge hadi akome”
“haaaha, na ule weusi lazima wamtengenezee carolaiti ya tura”
Sote tukajikuta tukicheka kwa furaha kwani, mazungumzo ya hawa jamaa yamenifanya nijihisi mchangamfu gafla
“unajua yule ndio chanzo cha mimi kupelekwa jwtz?”
“weee”

“mama vile, si alikuwa anajiona mbabe.Sasa nilivyo mpiga ile siku ticha akaniita ofisini kwake na kunihoji hoji maswali, akaniambia tangu aanze kufundisha haijawahi kutokea afande wa kike kumpiga afande wa kiume”
“ila alikupa kabahati”
“kiupande mmoja ninamshukuru, kwa maana alinisaidia sana”

“sisi bwana, bado tunakula ngwamba na wananchi, nakuona wewe upo kitengo kikubwa, hadi munatembelea na v8?”
“dulla hembu acha utani?”
“kweli dore unadhani ni utani? Sisi tumesha telekezwa, tunakazi ya kutembelea vidifender hivi vilivyo choka, kila siku vinakazi ya kushinda gereji”
“ahaaaa dulla wewe ropoka usikiwe, utahamishiwa kitivo huko ukale makabichi”

Sote tukabaki tukiwa tunachekea kwa sauti ya juu hadi baadhi ya askari walio karibu nasi wakawa na kazi yakutushangaa
“kwenye ukweli, inatubidi tuzungumze”
“ni kweli, ila mmmmmm”
“jamani, naona tukikaa sana hapa, hamuta enda lindo sisi ngoja tusepe”

“kwani, munakwenda wapi muda huu?”
“tunataka twende pande, jeshini”
“mbona usiku, chukueni hoteli mulale, asubuhi na mapema mudimke”
“etii?”
“hakuna cha etiii, njia hiyo usiku sasa hivi sio nzuri”
“kuna majambazi?”
“mara mia kungekuwa na majambazi”
“ila?”

“kuna vituko vya ajabu, unaweza kukuta watu wanakatiza barabarani wakiwa na kanzu huku wanakwenda kuzika, ukisema uwapige risasi, kesho unakufa”
“mmmmm”
Ilinibidi nigune
“kaka eddy wala usigune, hii ndio tanga bwana, ukicheza vibaya wala humalizi siku”
“sasa hapa ni wapi kwenye hotel nzuri?”
Dorecy aliuliza

“zipo nyingi, ni pesa yako tuu”
“maeneo gani zipo?”
“chuda si unapapata?”
“ndio?”
“sasa, ule mtaa ukikosa sehemu ya kulala ujue unabahati mbaya”
“sawa jamani, ngoja tuondoke, nikisema tuendelee hapa tutakesha”

“umeona eheee”
“nishidaaa”
“jamani, tutaendelea kuwasiliana”
“tunawasiliana vipi wakati hatuna hata namba za simu ulizo tuachia”
“simu sina”
“haaaa, unaishije bila simu?”
“nitachukua kesho”

“sikia chukua simu yangu, mukifika sehemu mutakapo pata chumba utatujulisha, si unajua wewe sasa hivi ni mtu mkubwa kwetu, shemeji samahani bwana kwa kuipendekaza kumkabithi simu bibie, usije ukanihisi vibaya”
“hamna shida, ndugu zangu pia mutakuwa mumetusaidia sana”

“ndio maana nimekukubali shem wangu, ingekuwa jinga lengine hapa lingevuta mdomo kama yule bibi tuliye mkamata jana ameanguka na ungo wao wakichawi”
“eheee, hayo mengine tena, mumeanza kukamata hadi wachawi?”

Dorecy aliuliza
“ohoo, shosti huu mji bwana ahaaa, juzi kati maeneo ya mwakizaro huko, tulipewa taarifa kuna bibi ameanguka na ungo, acha wananchi wamabamize mawe.Sasa sisi tukaitwa kumchukua, mwanagu kabibi kaze japo kamepigwa ila hakajafa, sasa huo mdomo alivyo uvuta mbele kama anapiga busu la karne”

Jamaa alizungumza na kuzidi kutufanya tucheke kwani alitoa mfano wa jinsi bibi huyo alivyo uvuta mdomo wake mbele
“john unafanana naye”
“dullah hembu acha ujinga bwana”
“hahaaa, jamani ngoja tuondoke”
“sasa utaondokaje pasipo mimi kukuambia namba gani unipigie”

“haya mwaya, niambie”
John akachukua simu aliyo mpa dorecy, na kuandika namba na kumuonyesha dorecy
“haaaaa....!!”
Dorecy alihamaki
“nini?”
“mbona mba mbaya hivi, kama amba za majeneza”
“ahaaa dore sasa hizo dharau”
“ahaaa kwa hiyo john na wewe unanunaga?”
“hapanaaa”

“unazani atanuna, anaogopa ukamfanaya kama shosti yake nyandeza”
“jamani, hembu achani utoto, hapa mume wangu ana njaa ngoja twende sehemu tukale kwanza kisha nitawapigia simu sehemu muje tunywe kidogo”
“mambo si ndio hayo”
“nyooo, john ndio maana pesa yako ya marupurupu unaimalizia kwenye pombe”
“ahaaa nina shida gani, sina mke wala mtoto, acha niuponde ujana”
“john hadi sasa hivi huna mtoto!?”

“wewe unaye?”
Dorecy akizungumza
“ahaaa haya bwana, kwa herini”
“sawa, bro eddy mkumbushe bwana huyo kuja kunywa kidogo, si unajua tena katikati ya mwenzi huu, hali mbayaa”
“powa kaka zangu, tupo pamoja”
Niliwajibu, dorecy akafunga mlango wa gari na kuanza kuondoka taratibu,
“tunaelekea wapi?”
“kuna, hiteli hapo mbele inaitwa nyinda anex ngoja nikacheki kama tutapata chumba”
“powa, hivi wale rafiki zako wanafanya kazi kweli?”
“ahaaa, wale ni pumba, ningesema nikae nao pale.Tungekesha”

Tukafika kwenye hoteli aliyo niambia, dorecy akashuka kwenye gari na kuniomba nimsubiri.Nikageuka siti ya nyuma na kukikuta kibegi changu cha madini, nikakifungua ndani na kukuta kikiwa kama kilivyo, hakuna kitu hata kimoja kilicho pungua.Dorecy akarudi na kuingia ndani ya gari.

“vipi umepata?”
“vyumba vimejaa”
“ahaa, mkosi huo”
“ngoja twende, hapo mbele kuna hotel ya ghorofa tuliipita”
“powa, alafu bastola zangu zipo wapi?”
“fungua hapo, pembeni utaziona”

Dorecy akanielekeza, nikafungua sehemu ya pembeni yangu kwenye siti na kuzikuta zote mbili, nikazichukua na kuzichomeka kwenye viatu, tukafika kwenye hotel moja inayo itwa mtendele.Kama kawaida dorecy akashuka na kuniacha kwenye gari, akaingia na baada ya dadika tano akarudi akiwa ameshika funguo ya chumba mkononi.

“nimepata”
Nikashuka ndani ya gari huko nikiwa nimeshika kibegi changu chenye madini, na sote  tukaingia kwenye hoteli, hiyo iliyo tengenezwa vizuri kwa kwenda juu.Tukapandisha ghorofa ya tatu kilipo chumba chetu.

“eddy, hivi hicho kibegi kina nini?”
“nitakuambia, ila kikubwa kwanza, tuzungumze vitu vya maana”
“hata kuoga hatuogi?”
“tutaoga, kikubwa tuzugumze ni jinsi gani tutampata mzee godwin?”
“eddy, mzee godwin anamtandao mkubwa sana, tena sana.Sio mtu wa kumuendea kichwa kichwa, wewe mwenyewe unaona jinsi alivyo kutia nguvuni, laiti ingekuwa sio mimi, sijui ungekuwa wapi hadi sasa hivi.”
“sawa, ila kuna vitu ambavyo nahitaki kuvifahamu kupitia wewe”
“uliza”

“hivi ni watu gani ambao, mzee godwin anashuhulika nao?”
“ahaaa, ni wazito serikalini, ukumbuke kwamba yule ni mtu mkubwa sana kwenye hii nchi, pili utambue ni mkuu wa jeshi, yaani akitoka raisi katika mamlaka ya jeshi anafwata yeye, so huyo sio mtu wa kusema unamuendea kichwa kichwa.Nilazima tuwe na mipango ambayo itatufanya tuweze kumpata mama kwanza, kisha hao wengine watafwata”
Nikashusha pumzi zangu huku ninamtizama dorecy kwa umakini machoni.

“eddy, lengo la mimi kukuleta huku ni wewe kwanza ukapate kwanza mazoezi ya kijeshi, japo wewe mwenyewe unajiona umekamilika ila bado, tena sana”
Dorecy alizungumza huku akinitazama machoni
“kwani kupambana na mtu kuna ulazimu wa mazozi ya kijeshi?”
“ingekuwa sio hivyo basi hata wauza mitumba wangeenda kupigana vitani”
Jibu la dorecy likabaki likinipa msongamano wa mawazo
“ila huoni kama baba atajua?”
“baba gani?”
“mzee godwin”

“ahaaa, huko ninapo kupeleka mimi, atakaye jua ni mimi na huyo ndugu yangu ninaye mfwata huko”
Dorecy alizungumza kwa kujiamini sana
“sawa nimeku.....”
Nikastukia dorecy akinivuta kwa nguvu na kuninyanyua kwenye sofa nililo kaa, nikastukia akinitandika kichwa cha uso kilicho niyumbisha huku nikiona giza kwenye macho yangu, zikiambatana na nanenane
“ahaaa”

Niliropoka, ila nikastukia akinitandika ngumi mbili za kifua zilizo niangusha chini, nikachomoa bastola ya kwanza kwenye kiatu hata kabla sijaishika vizuri nikashtukia teke likitua kweny mkono wangu na kuiangushia mbali bastola, nikachomoa ya pili, hali ikawa kama hiyo hiyo ya kupigwa teke la mkono
“unanipigia nini, sasa”

Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga, nikajaribu kunyanyuka, ila nikaikuta miguu yangu ikipigwa na mguu mmoja wa dorecy, nikajikuta nikirudi chini tena.Kwa jicho langu moja nilamchunguza dorecy jinsi alivyo simama huku mikono yake akiwa ameikunja ngumi.

Nikasimama kwa haraka, dorecy akarusha ngumi, niliyo bahatika kuiona na kuikwepa.Kitendo cha mimi kuikwepa ngumi, nikastukia kigoti cha dorecy kikitua kifuani mwangu na kujikuta nikinyanyuka kwenda juu mithili ya mtu aliyepigwa shoti ya umeme, nikastukia ngumi moja kali ikitua kwenye komo langu na kunisabanisha kunirudisha kwenye kochi huku macho yangu nikiwa nimeyafumba baada ya kuiona ngumi nyingine ikinijia kwenye uso, nikaisikilizia ila haikufika kwa wakati muafaka ikanibidi kufumbua macho na kujikuta nimetazamana jicho moja la bastola aliyo ishika dorecy, huku ikiwa imesimama sentimita chache kutoka yalipo macho yangu.

“sali sala yako ya mwisho?”
Dorecy alizungumza huku sura yake ikiwa imejaa jasho jingi, na mikonjo iliyonifanya niamini huu ni mwisho wa maisha yangu mimi eddy godwin....
 
 Itaendelea.....

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!